Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha afya na sayansi shirikishi,Muhimbili (Muhas)Prof Appolinary Kamulabwa anayeshughulika taaluma,utafiti na ushauri katika chuo hicho akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki katika mbio za Muhas Fun Run (Reunion Fun Run).
KAIMU Mwenyekiti Chuo Kikuu cha Afya na sayansi shirikishi,Muhimbili (Muhas) Dkt khadija Malima akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki katika mbio za Muhas Fun Run (Reunion Fun Run).
SEHEMU ya washiriki
……………………………..
Watanzania wametakiwa kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuepukana na wimbi la magonjwa hasa yasiyo ya kuambukiza na uzito wa kupitiliza.
Hayo yamesemwa leo Novemba 26,2022 jijini Dar es salaam na naibu makamu mkuu wa chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi,Muhimbili (Muhas)Prof Appolinary Kamulabwa anayeshughulika taaluma,utafiti na ushauri wakati chuo hicho kilipofanya mbio za hiari/furaha kwa kushirikisha wahitimu waliowahi kusoma chuoni hapo miaka ya nyuma zijulikanazo kama (Reunion Fun Run).
Prof Kamulabwa amesema kuwa lengo la mbio hizo ni kukutanisha wahitimu hao waliosoma miaka ya nyuma na washirika wa chuo hicho Kufahamiana,kukumbushana na kuangalia walipo na kuangalia maendeleo ya Chuo hicho.
Amesema kuwa mbio hizo ambazo zilikuwa za kilomita 5,10 na 15 ambazo hufanyika mara moja kwa mwaka ambapo kwa mwaka huu mwitikio umekuwa mkubwa na kuongeza kuwa wahitimu wa chuo hicho katika miaka ya nyuma wamekuwa na mchango mkubwa katika kukisaidia chuo hicho ikiwa ni pamoja na kutoa nafasi za wanafunzi wa Muhas, kusomea kwa vitendo (field) katika taasisi za afya wanazifanyia kazi.
“Ujumbe mkubwa wa fun run ya leo ni kuzingatia afya,na kama mnavyojua sasa hivi kuna wimbi kubwa sana la magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama kisukari,shinikizo la damu,saratani na mengine yasiyo ya kuambukiza yanazidi na chanzo kikubwa cha magonjwa haya ni namna ya maisha tunayoishi,miili yetu hatuishughulishi,tunakula vyakula visivyofaa kwa hiyo ndiyo maana tunafanya hivi fun run ili kutoa ujumbe kwa jamii kuwa tujitahidi kufanya mazoezi”amesema Prof Kamulabwa.
Hata hivyo amewashauri wazazi kuwashughulisha watoto wao kwa kuwajengea utaratibu wa kufanya mazoezi kwani watoto wengi kwa sasa uzito wao hauendani na umri wao kutokana na kutoshiriki mazoezi na kula vyakula visivyokuwa sahihi hivyo ni wakati sasa kufanya mazoezi wakiwa mashuleni,majumbani ili kuepuka magonjwa mbalimbali.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Muhas Convocation Dkt Khadija Malima amesema kuwa kupita mbio hizo ambazo zilianzishwa miaka mitatu iliyopita zitaendelea kuunganisha wahitimu wa Chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili, Muhas na wamejipanga huko mbeleni kuanza kukusanya hela kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya chuo na kusaidia wasiojiweza kimatibabu ikiwemo wanafunzi wanaosoma chuoni hapo ambao wanafanya vizuri kamasomo na waliokosa mikopo
Aidha ameongeza kuwa katika Mbio za miaka ijayo chuo hicho pia kitaandaa mipango mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushirikisha pia jamii ambayo siyo wahitimu wa chuo hicho(Allumni) pamoja kutoa huduma ya upimaji wa afya,uzito,presha,kisukari na ushauri wa kiafya katika mbio za FunRun huku akitoa wito kwa jamii kulipa umuhimu suala la mazoezi ili kujenga afya zao.