Makamu Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu- Taaluma, Dk. Momole Kasambala akizungumza katika semina hiyo.
Wanafunzi wakishiriki kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale, Singida
TAASISI ya Uhasibu Tanzaia (TIA), Kampasi ya Singida imetoa semina kwa wanafunzi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kupunguza changamoto ya
upungufu wa ajira inayowakabili vijana wengi pale wanapomaliza masomo yao ya
elimu ya juu.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) , Prof. William
Pallangyo amesema semina hiyo ya Ujasiriamali itawasidai vijana hao
kuanziisha biashara mbalimbali watakapomaliza masomo yao.
Pallangyo alisema hayo wakati akifungua semina ya kuwajengea
uwezo wanafunzi wa Taasisi hiyo ya Uhasibu Tanzania namna ya kubuni mawazo
mbalimbali ya biashara, yatakayowasidia kujiajiri wenyewe na kuacha tabia ya
kusubiri kuajiriwa.
Alisema kumekuwa na ufinyu wa ajira katika sekta mbalimbali hivyo kupitia
mfunzo hayo ya ujasiriamali itasaidia kutambua fursa zilizopo.
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu- Taaluma, Dk. Momole Kasambala alisema Taasisi ya Uhasibu Tanzania imejipanga kutoa mafunzo hayo mara kwa mara kwa ajiliya kuwajengea uwezo wa kupata mawazo ya biashara ambayo yatawasiadia katika
kujiajiri.
Aidha Dk.Kasambala alisema wanafunzi wenye mawazo mazuri
watashindanishwa na mawazo yatakayoshinda
yatapelekwa mbele zaidi kwa kutafutiwa mitaji na kukutanishwa nataasisi za
kifedha ili wanafunzi hao waweze kupata mikopo ya kuanzisha biashara.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo wamesema
mafunzo hayo yatawasidia kuanzisha biashara zitakozowasaidia kuondokana na
changamoto ya upatikananji wa ajira.
Wamesema kupitia biashara hizo pia wataweza kuajiri vijana wengine ambao
hawana ajira na hivyo kuwasaidia vijana wengi waliomaliza vyuo na hawana ajira
kupata ajira nchini.
Hata hivyo wameomba taasisi za kifedha kuweka mikopo yenye riba nafuu
ambayo itawasiadia wao kukopa na kuanzisha biashara ambazo zitatoa ajira kwa
vijana wengi.