KAIMU Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo, Dkt. Asimwe Rwiguza ,akizungumza wakati akifungua kikao cha Maoni ya Wadau ya rasimu ya Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Mifugo ya Mwaka 2022 ,kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Shirika la Kilimo na Chakula Dunia ( FAO) ambaye pia ni kiongozi wa timu ya kuandaa Rasimu ya Sera Mifugo ya mwaka 2022 Dkt.John Laffa akitoa maelezo mafupi ya shirika la FAO linavyoshirikiana na wandaaji wa Rasimu ya Sera hiyo katika kuhakikisha wanalipia gharama za vikao vya kupitia sera hiyo vilivhokuwa vinafanyika ndani na nje ya Dodoma.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw.Venance Ntylundura akitoa maelezo mafupi ya historia ya kuanza kwa mchakato wa kuandika rasimu hiyo hadi hapa ilipofikia hii leo iko kwa wadau wanatoa maoni yao.
Katibu wa Chama Cha Wafugaji Tanzania Bw.Joshua Lugaso akitoa maelezo mafupi kuhusu kikao cha utoaji Maoni ya Wadau wa Mifugo wa rasimu ya Sera ya Mifugo kilichofanyika jijini Dodoma.
………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
KAIMU Katibu Mkuu sekta ya Mifugo Dkt. Asimwe Rwiguza amesema kuwa utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Mifugo kwa mwaka 2022 itawasaidia kuwa na sekta ya mifugo yenye tija inayoendeshwa kibiashara ambayo ni endelevu na yenye kuleta maisha bora kwa mfugaji mmoja mmoja lakini pia kwa taifa zima.
Hayo ameyasema jana jijini Dodoma Novemba 24 wakati alipokuwa akifungua kikao cha maoni ya wadau ya rasimu ya mkakati wa utekelezaji wa sera ya mifugo ya mwaka 2022.
Amesema mkakati huo utatekelezwa kwa miaka 10 kwanzia mwaka 2023 hadi 2033 na kwenye mkakati huo umeainisha hatua za kimkakati zitakazo chukuliwa kutekeleza matamko ya kisera ili kuweza kuifikia dira, dhamira na malengo ya sera ya mifugo ya mwaka 2022.
Amesema mkakati huo umebainisha gharama na mgawanyo wa majukumu kwa wadau mbalimbali, nakusema kuwa mkakati wa utekelezaji wasera ya mifugo umeainisha maeneo ya kimakakati ambayo ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa rasilimali za maeneo ya malisho ,kwani malisho ni changamoto kubwa kwa sasa na hasa katika kipindi hiki ambapo kunamabadiliko makubwa ya tabia ya nchi.
“ Lakini pia kuongeza uzalishaji na uhifadhi wa mbegu za malisho kuimarisha upatikanaji wa maji kwaajili ya mifugo, kuimarisha mnyororo wa dhamani wa mazao ya mifugo pamoja na masoko”amesema.
Lakini pia kwenye swala la la usalama wa chakula na lishe na hivo utakuwa umechangia kwenye uchumi wa nchi yetu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Mipango Venance Ntylunduru,amesema kuwa mchakato mzima wa kupata rasimu hiyo amesema kuwa iliandaliwa timu ya wataalam ambao ilichukua wadau kutoka mamlaka za serikali za mitaaa na wengine kutoka vyuoni na maeneo mengine ambayo walidhani itasaidia kutengeneza mkakati wa kutekeleza sera.
“Timu hiyo ilikaa ikaandaa rasimu ya mkakati wa utekelezaji na baada ya kupata rasimu ikaona vyema kuwaita wadau ili waweze kuipitia na kuona maeneo gani yanafaa yaboreshwe au maeneo gani yapo sawa kwaajili ya utekelezaji ili sekta ya mifugo iweze kusongambele kwa kadri inavyoongeza uzalishaji na tija”amesema.
Awali Mwakilishi wa Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) Dokta John Laffa amesema kuwa sekta ya mifugo inalaumiwa kuwa inamchango mdogo kwenye uchumi wa nchi kwamba ni asilimia 7.1
”Ukiangalia mchango wa sekta hii licha ya kuzalisha nyama na maziwa ambayo ni muhimu sana kupunguza utapiamlo kwa watoto na hata watu wazima lakini kupitia mbolea inaongeza tija kwenye kilimo.”amesema
Vilevile amesema kuwa sera hiyo imezingatia maoni ya wadau ambayo yamejumuishwa katika rasimu ya sera lakini pia imejumuisha maoni ya wafugaji na wataalam wa wizara.
“Mkakati huu unalenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa sera ya mifugo ,ambapo imeambatanishwa na mkakati wa kiuchumi”amesema.
Hata hivyo naye Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Joshua Lugaso amesema wanaposema ongezeko la mifugo siyo kwamba inaongezeka kwasababu ya sayansi ya mifugo kuwa nzuri nakuongeza kuwa wafugaji wa tanzania wanaendelea kubadilika siku hadi siku na ndio maana uzalishaji wa mifugo unakuwa mwingi.
“Wizara imejitahidi kutengeneza miundombinu mizuri ya matibabu na mambo mengine kwaajili ya ufugaji wetu”amesema.
Amesema kuwa sera hiyo inaenda kuangalia maeneo makuu matatu ikiwemo swala la maji,malisho na kumiliki ardhi ili kupunguza kuhamahama.
“Tukiboresha swala la maji kwa asilimia hata 70 inaondoa hii ya sasa kwani kila kiongozi wa nchi anasema mifugo inasababisha ukame kitua mbacho siyo kweli ingawa inasababisha lakini siyo kwa kiwango hicho kinachosemwa kwa sasa”amesema.
“Mabadiliko ya tabia ya nchi hayajaanza leo haya nimabadiliko tu hivyo isichukuliwe kuwa tanzania kuwa na mifugo mingi kunasababisha ukame mbona Kenya ambayo haina mifugo mingi ukame upo”amesema.