Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB,Bi. Ruth Zaipuna, akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya NMB, Bw.Benson Mahenya moja ya tuzo 18 za kitaifa na kimataifa katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NMB, Bw. Ramadhan Mwikalu na kulia ni Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw.Filbert Mponzi.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NMB wakiwa na Menejimenti ya NMB, katika picha ya pamoja wakiwa na baadhi ya tuzo ilizoshinda benki hiyo, baada ya kuzitangaza kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya NMB. Baadhi ya Tuzo kati ya 18 za kitaifa na kimataifa ilizotunukiwa Benki ya NMB.
*********************
Benki ya NMB imedhibitisha uongozi na sifa yake ya kuwa taasisi kinara wa huduma za kifedha nchini na isiyo kuwa na mpinzani, katika kulihudumia taifa baada ya kutwaa tuzo 18 za ubora za kitaifa na kimataifa.
Benki hiyo itametangaza kuwa, tuzo 10 za kimataifa imwetunukiwa hivi karibuni kwa kuwahudumia vyema wateja wake na watanzania wote kwa ujumla, pamoja na kuwa kinara wa ujumuishaji wa kifedha nchini. Nne kati ya tuzo hizo, zimetolewa kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bi. Ruth Zaipuna kwa kuwa kiongozi bora.
Akizungumza katika hafla ya kuzitangaza tuzo hizo, Bi, Ruth alizitaja baadhi ya tuzo hizo kutoka kwenye majarida ya kimataifa zikiwa ni pamoja na:
- Benki Bora Tanzania kwa mwaka 2022 – Kutoka Jarida la Global Brands Magazine
- Benki Bora ya Wateja Binafsi na Biashara – Kutoka Jarida la World Economic Magazine, Jarida la International Business Magazine na Jarida la Global Banking and Finance Review
- Benki Bora katika Kilimo Biashara – Kutoka Jarida la Global Brands Magazine
- Ubunifu Bora katika Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi Tanzania – Kutoka International Bankers Award
- Benki Bora kwa Wateja Maalum – kutoka International Bankers
- Afisa Mtendaji Mkuu Bora kwa Mabenki nchini Tanzania – kutoka Jarida la World Economic Magazine, Jarida la Global Brands Magazine na African Bank 4.0 Summit
- Hatifungani Bora ya Mwaka 2022 – kutoka Mtandao wa Mitaji kwa Wajasiliamali Wadogo na wa Kati ambao wameshirikiana na nchi za G20 na IFC.
Tuzo hizi kutoka majarida na taasisi zinazoheshimika duniani, zimeitambulisha Benki ya NMB kitaifa na kimataifa, hivyo basi, kuitambulisha sekta na nchi yetu kimataifa. Lakini pia, zinadhihirisha imani kubwa na heshima waliyonayo sokoni.
Kwa upande wa tuzo za kitaifa, NMB ilishinda tuzo tatu za Mamlaka ya Mapato (TRA) ikiwemo ile ya Mshindi wa Jumla ya taasisi zinazolipa kodi kubwa na kwa kuzingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi.
Akizungumza kabla ya kupokea tuzo hizo, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Bw. Benson Mahenya, alisema benki hiyo ina kila sababu ya kujivunia tuzo hizo, kwani ni matokeo ya kazi kubwa inayofanywa na manejimenti pamoja na wafanyakazi wote kwa ujumla. Aliongeza kua, mafanikio hayo yametokana na ubora na viwango vya kimataifa vya huduma zote zinazotolewa na Benki ya NMB pamoja na uendeshaji wake.