MWENYEKITI wa Tume ya Watumishi wa Umma Jaji Mstaafu Hamisa Kalombola,akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bw.Athuman Masasi,wakati wa ziara ya Makamishna kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bw.Athuman Masasi,akitoa taarifa ya miradi inayofanywa na halmashauri hiyo wakati wa ziara ya Makamishna ya kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika.
Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma Balozi Adadi Rajabu,akiwasisitiza jambo watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi wakati wa ziara ya Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma waliofanya ziara katika Wilaya hiyo.
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bw.Athuman Masasi,akiwaeleza jambo Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma waliofanya ziara ya kutembelea Miradi inayotekelezwa pamoja na Kujifunza na kuona namna Mashine za Kieletroniki za Ukusanyaji Mapato (POS) zinavyotumika na Mikakati iliyopo katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vyao.
MWENYEKITI wa Tume ya Watumishi wa Umma Jaji Mstaafu Hamisa Kalombola,akiwa na wajumbe wakiangalia namna Mashine za Kieletroniki za Ukusanyaji Mapato (POS) zinavyotumika katika Stendi ya Bahi wakati wa ziara ya Makamishna wa Tume hiyo katika Halmashauri ya Bahi.
MWENYEKITI wa Tume ya Watumishi wa Umma Jaji Mstaafu Hamisa Kalombola,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kujifunza na kuona namna Mashine za Kieletroniki za Ukusanyaji Mapato (POS) zinavyotumika katika Stendi ya Bahi wakati wa ziara ya Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bw.Athuman Masasi,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Makamishna wa Tume ya Watumishi wa Umma walipofanya ziara ya katika Halmashauri ya Bahi kutembelea na Kujifunza na kuona namna Mashine za Kieletroniki za Ukusanyaji Mapato (POS) zinavyotumika katika Vituo vyao.
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma Balozi Adadi Rajabu,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Makamishna wa Tume ya Watumishi wa Umma walipofanya ziara katika Halmshauri ya Wilaya ya Bahi.
…………………………………….
Na.Alex Sonna-BAHI
TUME ya Watumishi wa Umma imewakumbusha watendaji nchini kuwa waaminifu katika utendaji kazi hasa katika suala la kutumia Mashine za kielektroniki za Ukusanyaji Mapato ili kuepukana na changamoto za upotevu wa Mapato ya Serikali .
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Hamisa Kalombola,wakati wa ziara ya Makamishna ya kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma ambapo amesema changaomoto hizo za upotevu wa mapoto umepelekea kufukuzwa kazi kwa baadhi ya watumishi wa umma.
Jaji Mstaafu Kalombola amesema kuwa mtumishi wa umma ni lazima aweke mbele maslahi ya nchi kwamba hizi fedha wanazokusanya siziwe kwa matumizi binafsi ni kwa matumizi ya nchi nzima.
“Tumekuwa tukipambana na hali hiyo kwani kuna mashine ambazo zinatumika sasa kumekuwa na kasoro tumekuja kuzigundua.
“Unakuta wamefikishwa kwenye mamlaka ya nidhamu kutokana na kasoro ambazo zingeweza kuzuilika na hii inatokana na makusanyo yanakusanywa.
“Halafu fedha zinabakia kwa mkusanyaji wengine siku tatu mpaka nne kama binadamu wanajikuta wanaingia katika matatizo
“Kwa sababu anaingia katika vishawishi kwa kujisahau kwamba fedha hizo ni za Serikali na ni mali ya Serikali na inazitumia kwa maendelea,”amesema Jaji Mstaafu Kalombola
Amesema kuwa wamekuja katika Halmashauri ya Bahi kuwasisitizia watumishi kuhusu matumizi ya fedha za serikali yanaweza kuwapeleka katika shida.
“Tumekuja kusisitiza kuja kuhimiza cha msingi ni kuwa mwaminifu na huu ni wito kwa ajili ya wakusanya mapato wote Tanzania nzima,”amesema.
Aidha amezikumbusha Halmashauri pale ambapo mtumishi amefanya kosa basi taratibu sheria na kanuni ni lazima zifuate
“Nasisitiza taasisi na halmashauri wanapomshughulikia mtumishi inatakiwa wafuate taratibu na kanuni.Na inatakiwa ifanywe hivyo hata sisi tusibaki kuwa na majalada mengi ambayo yalikuwa hayana haja ya kufika kwetu.
“Waajiri wazingatie hizo taratibu kanuni na sheria na watumishi wafanye kazi sio kwa mazoea wafanye kwa kufuata taratibu na kanuni,”amesema
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bw.Athuman Masasi amesema wanaendelea na ukusanyaji wa mapato na kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanathibiti mianya yote ya utoroshaji wa mapato hayo.
“Kwa mfano ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mashine unahitaji uaminifu na uadilifu mtu anaweza asikate kama ambavyo amepaswa kukata.
“Na akakosa uaminifu kazi yetu kubwa tunafanya ukaguzi mara tunapokutana na watu wa namna hiyo hana risiti sahihi sisi tunapiga faini lakini huyu ambaye hakukata risiti nae tunaweka utaratibu wa kuwachukulia hatua,”amesema Bw.Masasi
Masasi amesema wanaishukuru Serikali kwa kufanya jitihada za kuhakikisha kunakuwa na mifumo ya ukusanyaji mapato.
“Jukumu letu sio kulala na kusubiri mtu akusanye pia ni na kwenda kumfuatilia huko huko,”amesema
Naye Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma Balozi Adadi Rajabu amesema kumekuwa na rufaa nyingi ambazo watumishi wamefukuzwa kutokana na mfumo wa POS Mashine.
“Sisi kama Tume tumeona ngoja tungalie hili tatizo na Tamisemi wamegundua hilo lakini wanakuja na mfumo mwingine wa Tausi utatatua haya matatizo ambayo yameonekana,”amesema Balozi Rajabu
Katika Ziara hiyo wamezungumza na watumishi pamoja na kutembelea Miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya Bahi na kuwatembelea Watendaji wa Vijiji kwa lengo la Kujifunza na kuona namna Mashine za Kieletroniki za Ukusanyaji Mapato (POS) zinavyotumika na Mikakati iliyopo katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vyao.