KAMPUNI ya Geita Gold Mining Ltd. (GGML) imetambuliwa kwa mara nyingine tena kama mlipa kodi wa viwango vya juu katika sekta ya madini kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Tuzo hizo zilipokelewa mwishoni mwa wiki na Meneja Mwandamizi wa Fedha kutoka GGML, Ikingo Gombo (kulia) na Meneja Utatuzi wa Migogoro ya Kodi kutoka GGML, Godvictor Lyimo(katikati) kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano, Nape Nnauye, (kushoto).
Pia imetambuliwa kama kampuni iliyozingatia kiwango bora cha thamani ya bidhaa zilizosafirishwa nje ya nchi mwaka 2021/2022. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Chande (kushoto) alikabidhi tuzo hiyo kwa Meneja Mwandamizi wa Fedha kutoka GGML, Ikingo Gombo (katikati) na Meneja Utatuzi wa Migogoro ya Kodi Godvictor Lyimo kutoka GGML.