Na Dotto Mwaibale, Singida
SERIKALI imewataka Wakurugenzi wa
Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa mikoa kuacha tabia ya
kujihusisha na vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa mali za Umma na kusimamia
maadili ya watumishi wa Umma kwa ajili ya kutoa ufanisi wa kazi ili malengo ya
serikali yaweze kutimia.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George
Simbachawene ameyasema hayo mkoani Singida wakati akifunaga mafunzo ya
kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki, Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu
Tawala Wasaidizi wa Mikoa.
Waziri Simbachewene pia amewataka kwendaKusimiamia majukumu yao kwa weledi
na ufanisi na kusimamia maadili ya watumishi ili ufanisi wa kazi uonekene kwa
watumishi hao.
Aidha Waziri Simbachawene amewakumbusha majukumu yao mahala pao pa kazi ni
kwenda kusimamia taratibu na sheria zilizopo katika maeneo yao.
Akizungumza katika ufugaji wa mafunzo hayo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel
alisema, mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza weledi wa utendaji kazi wa
Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa.
Baada ya mafunzo haya, baadhi ya washiriki wanasema makosa madogo madogo
yaliokuwa yanajitokeza kwenye masuala ya itifaki yatapungua kwa kiasi kikubwa.
Mafunzo haya ya siku mbili ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki kwenye
matukio ya Viongozi wa Kitaifa, kwa Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu
Tawala Wasaidizi wa Mikoa yanafanyika mkoani Singida kufuatia kuwepo kwa
changamoto za kiitifaki kwa viongozi hao pale viongozi wa kitaifa
wanapotembelea katika maeneo yao.