DIWANI wa Kata ya Chumbageni (CCM) akizundua kambi maalumu katika kituo cha Sayansi cha Kisosora Jijini Tanga (Stem Park) ambayo itawezesha wanafunzi kujifunza namna ya kutumia sayansi kwa ajili kutatua matatizo kwenye Jamii kila siku. kulia ni Mkurugenzi wa Mwanzilishi wa Project Aspire Dkt Lwidiko Edward
Mkurugenzi wa Mwanzilishi wa kituo cha Sayansi cha Kisosora Jijini Tanga (Stem Park) Project Aspire Dkt Lwidiko Edward akizungumza wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Ofisi wa mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi Marekani nchini Chad Moris
Mkurugenzi wa Mwanzilishi wa kituo cha Sayansi cha Kisosora Jijini Tanga (Stem Park) Project Aspire Dkt Lwidiko Edward akizungumza jambo kwa wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi huo
Na Oscar Assenga,TANGA.
ZAIDI ya wanafunzi 120 wa shule za Sekondari Jijini Tanga wameanza kambi maalumu katika kituo cha Sayansi cha Kisosora Jijini Tanga (Stem Park) ambapo watakuwa wakijifunza namna ya kutumia sayansi kwa ajili kutatua matatizo kwenye Jamii kila siku.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kambi hiyo,Mkurugenzi wa Mwanzilishi wa Project Aspire Dkt Lwidiko Edward alisema lengo kuanzishwa kwake ni kuhamasisha na kubadilisha utamaduni wa kujifunza masomo ya sayansi,tekonolojia ya uhandisi na mahesabu.
Alisema wanafunzi hao watakuwepo hapo kwa wiki nzima watakuwa wakijifunza namna tofauti ya kutatua matatizo kwa kutumia sayansi, teknolojia, uhandisi na mahesabu na watakuwa wakiangalia kilimo cha kisasa kilimo janja.
Mkurugenzi huyo alisema umuhimu wa kambi hiyo ni muhimu hususani kwa watoto ni kuanza kuwafikirishwa kwamba masomo wana yofundishwa darasani yanaweza kutumika kutatua matatizo yaliyopo kwenye Jamii kila siku.
Alisema kwa hiyo kuwajengea uwezo kuwa wabunifu wenye uwezo wa kutatua matatizo yaliyopo kwenye jamii kwa namna tofauti ambavyo hawajifunzi wakiwa darasani.
“Wakati ituo can sayansi kilipoanzishwa mwezi Mei mwaka 2021 mpaka sasa tumefanikiwa kuwafikia wanafunzi 9400 ambao kila siku tunapata wanafunzi wapya 120 hadi 100 wapo wanaokuja na kuondoka” Alisema.
Hata hivyo alisema masomo ya sayansi ni magumu lakini haya kwepeki na jambo muhimu ni namna ya kuwafundisha sayansi watoto ili wanapojifunza kwa namna inavyoweza kuleta mantiki na wafanya kazi na walimu.
Mkurugenzi huyo alisema wanayansi ndio wanaoendesha dunia na Tanzania inahitaji wanasayansi wengi na Teknolojia ,wahandisi na wana mahesabu kwa ajili kuendesha nchini hivyo wanachokifanya ni kuchangia ongezeko hilo.
Awali akizungumza Ofisi wa mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi Marekani nchini Chad Moris alisema mradi huo ni muhimu kwa Taifa na ndio maana waliona umuhimu wa kutoa fedha dola za kimarekani 20,000 kwa ajili ya maendeleo ya kituo cha Sayansi ikiwa n i ujenzi lengo kuhakikisha Tanzania inapata wanasayansi wengi zaidi ambao watasaidia nchi katika maendeleo.