Meneja wa wakala wa Maabara ya
Veterinari Tanzania (TVLA) Kanda ya nyanda za juu kusini Dkt.Qwari Bura akiongea na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya miaka kumi ya TVLA.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
WAKALA wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA)
imewahimiza wafugaji kuzingatia matumizi sahihi ya chanjo za Mifugo na kuhakiki
wa ubora wa vyakula ili kuepusha madhara makubwa ya kiafya yanayoweza
kuwakabili walaji wa nyama hizo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
wiki ya maadhinisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa TVLA, Meneja TVLA Kanda ya
nyanda za juu kusini Dkt.Qwari Bura alisema kuwa matumizi yasiyo sahihi ya
chanjo na vyakula vya Mifugo yasipozingatiwa inatajwa huenda ikasababisha vifo
kutokana na madhara ya nyama ambayo italiwa na binadamu.
Dr Bura alisema kuwa matumizi
holela ya dawa hasa dawa za aina ya antibaiotiki huweza pia kuathiri binadamu
kutokana na kula mabaki ya dawa hizo kwenye vyakula vinavyotokana na wanyama.
Alisema kuwa hilo ni tatizo
kubwa linaloikabili dunia kwa sasa na wafugaji wanapaswa kuzingatia ushauri
unaotolewa ili kulidhibiti. Inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 2030, watu zaidi
ya milioni 10 watakufa kila mwaka kutokana na dawa kushindwa kuwatibu kwani
vimelea vya magonjwa vitakuwa vimejenga usugu unaotokana na matumizi holela ya
dawa kwa binadamu na mifugo.
Dr Bura alisema kuwa wafugaji
wanapaswa kuacha mara moja tabia ya kutibu wanyama wao bila vipimo ili kulinda
afya ya wanyama na binadamu
Dr Bura alisema kuwa Wakala ya Maabara ya
Veterinari Tanzania (TVLA) ni Wakala ya Serikali chini ya Wizara ya Mifugo na
Uvuvi iliyoanzishwa kwa Sheria ya Wakala za Serikali Na. 245 (iliyofanyiwa
marekebisho Mwaka 2009) na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe 9
Machi 2012. Wakala ilizinduliwa rasmi tarehe 11 Julai, 2012 na Katibu Mkuu
Kiongozi ilitokana na kuunganishwa kwa iliyokuwa Maabara Kuu ya Mifugo (CVL),
Vituo vya Kanda vya Uchunguzi na Utambuzi wa Magonjwa ya Mifugo (VICs), Taasisi
ya Utafiti wa Ndorobo (TTRI) Tanga na Kituo cha Utafiti wa Ndorobo (TTRC)
Kigoma.
alisema kuwa wakala wanavituo 11 ambavyo
hutekeleza majukumu mbalimbali ya Wakala katika maeneo yao ambavyo ni Taasisi
ya Chanjo Tanzania (TVI) – KIBAHA-PWANI ambayo kazi yake pekee ni kufanya
tafiti za chanjo na kuzalisha chanjo za mifugo. Maabara ya Veterinari Kanda ya
Kati – DODOMA Maabara ya Veterinari Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini –
IRINGAMaabara ya Veterinari Kanda ya Ziwa – MWANZA Maabara ya Veterinari Kanda
ya Kaskazini – ARUSHA Maabara ya Veterinari Kanda ya Magharibi – TABORA Maabara
ya Veterinari Kanda ya Kusini – MTWARAMaabara ya kanda ya Kusini
Magharibi-SUMBAWANGAMaabara ya Kanda ya Ziwa MEATU – SIMIYU. Kituo cha utafiti
wa magonjwa yaenezwayo na wadudu kwenye mifugo – VVBD – KIGOMA Kituo cha
utafiti wa magonjwa yaenezwayo na wadudu kwenye mifugo – VVBD- TANGA.
Dr Bura alisema kuwa watafungua Jengo Jipya la
Maabara na Ofisi Kituo cha Iringa kinachohudumia Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
ambayo ni mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na Ruvuma, wafugaji wa kuku wa asili
na kufanya mikutano na wafugaji kwa lengo la kutoa Elimu kuhusiana na huduma
zinazotolewa na TVLA hususan huduma za upimaji wa mgaonjwa na chanjo na Kufanya
upimaji wa magonjwa ya Mifugo (Bure) kwenye kituo chetu cha zamani kilichopo
mtaa wa Boma Manispaa ya Iringa na Uchanjaji wa kuku (Bure) kwenye kata
Alisemakuwa wakala ikaamua kufanya maadhimisho
ya miaka hiyo 10 tangu ilivyoanzishwa kwa kutenga siku tano kuanzia tarehe
21/11/2022 hadi tarehe 25/11/2022 kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa na lengo
la kuwafikia wafugaji na kurudisha kile ilichokipata kwa jamii. Maadhimisho
haya yatafanyika nchi nzima kwenye vituo vyetu vya Makao Makuu na vituo 11 vya
mikoani, na kila kituo kimepanga kufanya shughuli mbalimbali katika siku hizo
tano kama kwa Kutoa Elimu kuhusiana na
huduma zinazotolewa na TVLAKufanya upimaji wa magonjwa ya Mifugo (Bure) kwa
maeneo yatakayobainishwaUchanjaji wa Mifugo (Bure) kwa maeneo
yatakayobainishwaUtoaji wa Elimu ya Mifugo (Bure).
Dr Bura alimazia kwa kusema kuwa
Katika kufanikisha maadhimisho haya Kituo cha Iringa kimejipanga kuwaelemisha
wafugaji hususani juu ya shughuli ili kuongeza tija katika ufugaji Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini, shughuli hizo ni pamoja na elimu kuhusiana na Uchunguzi
na utambuzi wa Magonjwa ya Wanyama, elimu ya matumizi sahihi ya Chanjo za
Mifugo, umuhimu wa uhakiki wa Ubora wa Vyakula vya Mifugo, elimu kuhusu uhakiki
wa ubora, Usajili na uthibiti wa ubora wa viuatilifu vya Mifugo, na kutoa
huduma za ushauri na mafunzo.