Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango pamoja na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Anthony wa Padua Jimbo katoliki Tanga leo tarehe 20 Novemba 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na waumini wakatoliki mkoani Tanga mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Anthony wa Padua Jimbo katoliki Tanga leo tarehe 20 Novemba 2022.
**************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa wananchi mkoani Tanga kuhakikisha wanalinda amani iliopo kwa kuwabaini na kutoa taarifa za wale wote wanaoingia katika mkoa huo kwa lengo la kufanya uhalifu.
Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 20 Novemba 2022 mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Anthony wa Padua Jimbo katoliki Tanga, ibada ilioongozwa na msimamizi mkuu wa Jimbo hilo Padre Thomas Kiangio.
Amesema Jiographia ya mkoa huo inatumika kama njia ya kupokea watu mbalimbali ambao kati yao wapo wanaofanya uhalifu.
Pia Makamu wa Rais ametoa wito kwa waumini pamoja na wananchi wa Tanga kwa ujumla kuendelea na jitihada za kulinda mazingira ili kuepukana na athari zinazoendelea kujitokeza hivi sasa ikiwemo ukosefu maji pamoja na upungufu wa chakula.
Amewasihi viongozi wa dini kuendelea kuwasisitiza waumini juu ya maandiko matakatifu yanayoagiza kuilinda dunia ikiwemo kutunza mazingira.
Makamu wa Rais amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuwa chachu ya amani iliopo nchini pamoja na kuwasihi kuendelea kuwaombea viongozi ili waweze kuongoza taifa kwa hekima ya Mungu.
Makamu wa Rais yupo ziarani mkoani Tanga ambapo anakagua shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.