MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC),Livingstone Lusinde,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 20,2022 jijini Dodoma wakati akimataka Mbunge wa Kuteuliwa Dk.Bashiru Ally na kumtaka ajiuzulu ubunge.
……………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC),Livingstone Lusinde,amemshukia Mbunge wa Kuteuliwa Dk.Bashiru Ally na kumtaka ajiuzulu ubunge kwa kuwa hatendei haki uteuzi aliopewa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza leo Novemba 20,2022 jijini Dodoma na na waandishi wa habari Mhe.Lusinde,amesema amepokea kwa masikitiko kauli ya Dk.Bashiru kama yangesemwa na mwanachama wa kawaida wa CCM nisingemjibu, mtu mwenye viapo vingi ana mambo mengi ya nchi hii ni lazima nimjibu.
“Bashiru anataka Rais asipongezwe anakerwa na neno la Rais anaupiga mwingi, akawataka wakulima waungane kwa kuwa watawala hawawezi kuwa na amani, na wanashiba kutokana na nguvu ya wakulima,”amesema Mhe.Lusinde
Amesema kuwa huyu ni Mbunge ni wa kuteuliwa,kwa maana jimbo lake yeye ni Ikulu,sasa inashangaza kuona hakuna siku ameisifia Ikulu iliyomteua ambayo ni serikali kwa kazi nzuri inayoifanya.
“Mimi ni Mbunge wa Jimbo Kuna wakati kama serikali haijafanya vizuri naamka kuwatetea wananchi wangu lakini yeye Jimbo lake ni Ikulu, Mimi namshauri kwa kuwa anajisikia kichefuchefu Ikulu ikitajwa vizuri anatakiwa ampe nafasi Rais ya kuchagua Mbunge mwingine atakayemuelewa Rais,”amesema Lusinde.
“Nashangaa anatufundisha nini kwa sababu sisi watanzania serikali yetu haina dini lakini sisi tuna dini hata kwenye dini tunatakiwa kumshukuru Mungu, ukipata watoto mapacha au usipopata unashukuru, lakini Dk anatuambia utamaduni huo tuuache wakati huu wa Samia, tusimshukuru kwa kazi kubwa anayofanya,”
Kauli ya Lusinde inafuatia baada ya Dkt Bashiru kuzungumza kwenye mkutano wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania(MVIWATA),alionyeshwa kukerwa na wanaosifia utawala kwa kutumia neno anaupiga mwingi na kuutaka mtandao huo usiwe sehemu ya kusifia.