Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha ,Missaile Musa akizungumza katika hafla hiyo ya upokeaji miche ya miti mkoani Arusha.
**********************
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Kanisa la Yesu kristo la watakatifu wa siku za mwisho limekabithi miche ya matunda 30,000 kwa uongozi wa mkoa wa Arusha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi .
Akizungumza wakati wa kukabithi miche hiyo ya matunda ,Rais wa kanisa hilo,John Kasongo amesema kuwa, kanisa hilo limefikia hatua ya kutoa miche hiyo ya matunda kwa ajili ya kusaidia maswala ya usalama wa chakula kwa mkoa wa Arusha.
Amesema kuwa ,kanisa limekuwa likisaidia maswala mbalimbali ya kijamii katika.mikoa mbalimbali ikiwemo elimu,afya na maswala ya usalama wa chakula .
Ameongeza kuwa, kwa mkoa wa Arusha ndo wameanza kutoa misaada ambapo kwa kuanzia wameanza na kugawa miti matunda baada ya hapo watasaidia masala ya elimu kwa shule za serikali zenye uhitaji mbalimbali lengo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuchangia swala la maendeleo.
“Kama kanisa tumekuwa tukisaidia shughuli za maendeleo katika mikoa mbalimbali ambapo tumeshasaidia mkoa wa Dodoma na kwa hapa Arusha baada ya kukabithi miti tuna mpango wa kusaidia maswala ya elimu katika shule za serikali “amesema .
Amesema kuwa,kwa upande wa maswala ya chakula wamekuwa wakitoa chakula endapo kunatokea majanga ya vita kwa ajili ya kusaidia wahanga kuweza kuondokana na changamoto mbalimbali.
Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Missaile Musa amesema kuwa wanashukuru kanisa kwa namna ambavyo wameona uhitaji uliopo wa miche ya matunda na kuweza kutoa kwa ajili ya kusaidia mkoa wa Arusha .
Amesema kuwa,miche hiyo ya matunda itasambazwa katika shule na taasisi mbalimbali za mkoa huo kwa ajili ya kutunza mazingira na kuweza kupata miti ya kivuli kukabiliana na ukame na kupata matunda pia,ambapo amesema bado wana uhitaji wa miche zaidi kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali.
Kwa upande wa baadhi ya wadau waliokabithiwa miti hiyo,walisema kuwa kanisa hilo limetoa miti katika kipindi ambacho mkoa wa Arusha una uhitaji mkubwa wa kupanda miti kutokana na kuwepo kwa ukame uliosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi katika maeneo mengi hivyo miti hiyo itasaidia sana kurudisha kijani katika mkoa wetu.