Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inawajulisha wananchi kuwa kwa Mujibu wa Sheria ya Ardhi (SURA ya 113) kifungu cha 44 kila mmiliki wa Ardhi anatakiwa kutimiza masharti ya umiliki ikiwa ni pamoja na sharti la kulipa kodi ya pango la ardhi kila mwaka.
Aidha, baadhi ya wamiliki wamevunja sharti hilo Kwa mujibu wa kifungu cha 45 la kulipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati.
Hivyo, ninatoa taarifa kwamba, wananchi wote wanaodaiwa kodi ya pango la ardhi wanapewa nafasi ya mwisho kulipa kodi ya pango ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya tangazo hili. Baada ya muda huo kupita taratibu za kisheria za ubatilisho wa miliki zitaendelea.
IMETOLEWA NA DR. ALLAN KIJAZI KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI