Na Mwandishi wetu, Babati
UVCCM Mkoa wa Manyara, imepata Mwenyekiti mpya ambaye ni Inyas Stanslaus Amsi aliyerithi mikoba ya Mosses Komba.
Amsi ameshinda nafasi hiyo baada ya uchaguzi huo kurudiwa kwani awali hakupata zaidi ya nusu ya kura za wajumbe.
Awali, wagombea walikuwa wanne waliochuana ambao ni Haula Seif, Starnley Charles Loti Lembrice na Inyas Hams ila wagombea wawili Loti Lembrice na Inyas Hams ikabidi warudie mchuano wao.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dkt Suleiman Hassan Serera ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi huo ametangaza matokeo hayo kuwa Hams ameshinda kwa kura 271 na Lothi Lembris kura 176.
Dkt Serera amemtaja mshindi wa nafasi ya ujumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa ni Christine Seena Millya aliyepata kura 224 kwa kuwashinda Josephine Akonaay aliyepata kura 155 na Zumrath Salum aliyepata kura 61.
Amemtaja mshindi wa nafasi moja ya mjumbe wa mkutano mkuu UVCCM Taifa ni Clara Hauli.
“Mjumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM Mkoa ni Michael Rajab Daggo na mjumbe UVCCM kuwakilisha UWT Mkoa ni Lucy S Fisoo,” amesema Dkt Serera.
Amesema mjumbe wa UVCCM kuwakilisha wazazi Mkoa ni Elisante A. Tsuhhai.