Pongezi hizo zilitolewa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Bw. Hamad Chande katika uzinduzi rasmi wa muungano huo ujulikanao kwa jina la Tanzania Energy co-insurance Consortium au Consortium ya mafuta na gesi uliofanyika juzi usiku kwenye hotel ya Johari Rotana jinini Dar es Salaam.
Bw Chande alisema kuwa umoja huo ni wa kwanza hapa nchini na serikali itaongeza pato la taifa kupitia ada za bima ambazo sasa zitabakia hapa nchini tofauti na zamani.
Alisema awali, uwezo mtaji wa kampuni mojamoja za bima nchini haukuweza kukidhi vigezo vya ada ya kinga dhidi ya vihatarishi na kufanya miradi mingi ya uwezekaji katika sekta hiyo kuingia mikataba na makampuni ya nje ya nchi.
“Kutokana na sababu hizom, pato la taifa upotea kwani fedha za ada ya bima uchukuliwa na makapuni ya nje kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha.
Kupitia umoja huu, sasa makampuni ya uwezekaji wa nje yataweza kukata bima zao hapa nchini ili kukikinga na vihatarishi katika sekta ya mafuta na gesi,” alisema Bw Chande.
Alifafanua kuwa muungano huo unaongeza uwezo wa kuhimili vihatarishi hivyo na kusaidia ubakishaji (retention)za fedha za ada nchini kwa maendeleo ya taifa.
“Uhitaji wa muungano huu ulianza uhitaji mwaka 2019 kuelekea mwaka 2020 baada ya miradi mikubwa kama East Africa Crude Oil Pipeline) wenye thamani ya Dola bilioni 3.5 na mradi wa LNG (Gas Processing Plant) wente thamani wa dola za Kimarekani Bilioni 30, miradi mikubwa ya madini na kilimo.
Kutokana na thamani ya miradi hiyo kuwa kubwa, bima ya kinga dhidi ya vihatarishi ulipelekea uhitaji wa bima mtawanyo ambayo kwa asilimia kubwa ilinunuliwa kwa kampuni ya bima mtawanyo za nje na hivyo kupelekea fedha nyingikama malipo ya ada ya kukinga miradi hiyo dhidi ya vihatarishi kuzinufaisha nchi hizo,”alisema Bw Chande.
Alisema kuwa “Kutokana na mtaji mdogo wa makampuni ya hapa nyumbani, ilipelekea uhitaji wa kuundwa kwa umoja huo ili kuunganisha uwezo wa kampuni za ndani dhidi ya vihatarishi maalum ili kuweza kuhimili vihatalishi hivyo na kubakisha ada na kuongeza pato la Taifa,” alisema.
Kwa upande wake, Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt Baghayo Saqware alisema kuwa umoja huo unazifanya kampuni hizo 22 kuunganisha mitaji na kuwa na uwezo wa kuhimili vihatarishi vya miradi hiyo mikubwa pamoja na mradi gesi asilia wa Lindi wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 30 ambao unatarajiwa kutekelezwa hivi karibuni.
Bw Saqware alisema kuwa muunganiko huo utaleta faida mbalimbali kama kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha na kitaaluma kwa kampuni za bima, kuongeza uhifadhi wa ndani na uendeshaji mzuri wa hatari miongoni mwa kampuni za bima na bima mtawanyo, kulinda maslahi ya watanzania na kuongeza uwezo wa ndani kulingana na mahitaji ya kisheria (local content requirement) na kuongeza ajira.
Alisema faida nyingine ni kutoa mpangilio wa haki, uwazi na wenye usawa kwa kushirikisha wadau wengine wa bima katika sekta ya mafuta na gesi na kuongeza ujuzi na utaalam wa kuandikisha bima ya vihatarishi maalum kwa kupitia uzoefu utakaopatikana katika umja huo wa mafuta na gesi.
Wakati huo huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bima ya Phoenix AssuranceBw Ashraf Musbally alisema kuwa ndani ya wiki chache zijazo watatoa muongozi kwa wadau mbalimbali kuhusiana na malengo yao ya muda mfupi na mrefu.
Bw Musbally alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kuona wazo lao limeungwa mkono na wadau wa sekta hiyo na wanaamini litaleta tija katika maendeleoya sekta ya bima hasa kwa upande wa gesi na mafuta.