Mhe. Waziri Mbarawa akiambatana na Mkurugenzi wa Benki ya Afrika akipokea maelezo kuhusiana na chuo cha bahari kutoka kwa Ndugu Lusajo Martine katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 15 wa wadau wa Uchukuzi na usafirishaji uliofanyika Novemba 16 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 15 wa wadau wa Uchukuzi na usafirishaji uliofanyika Novemba 16 Jijini Dar es SalaamWaziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa akitoa neno la ufunguzi katika mkutano wa 15 wa wadau wa Uchukuzi na usafirishaji uliofanyika Novemba 16 Jijini Dar es Salaam
**********************
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa ametembelea Banda la chuo cha bahari Dar es Salaam katika maonesho yaliyoambatana na mkutano was 15 wa wadau wa sekta ya uchukuzi uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga LAPF Novemba 16 Jijini Dar es Salaam
Katika banda la chuo cha bahari Dar es Salaam, Waziri Mbarawa akiambatana na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika alipata maelezo kuhusu kozi mbalimbali zitolewazo na chuo hicho pamoja na fursa zitokanazo na bahari.
Ndugu Lusajo Martine alimueleza Mhe. Waziri kuwa Chuo cha Bahari Dar es Salaam kimeendelea kujipambanua katika kufundisha masomo yanayohusu tasnia ya bahari kwa wanafunzi kutoka Tanzania, Afrika Mashariki na Kati katika kiwango Cha kimataifa.