Waogeleaji wa timu ya Taifa ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
…………………………………..
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Waogeleaji 63 wa timu ya taifa ya Tanzania (Tanzanites na Diamond) kesho (Alhamis Novemba 17) wanaanza kampeni ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kanda ya tatu Afrika kwenye bwawa la klabu ya Dar es Salaam Gymkhana jijini.
Mashindano hayo yataanza saa 2.00 asubuhi na kushirikisha waogeleaji wengine 200 kutoka nchi nyingine 10 za bara la Afrika.
Nchi hizo ni Uganda ambayo itawakilishwa na waogeleaji 45, Burundi (10), Rwanda (14), Eritrea (5), Ethiopia (7), Zambia (23), Afrika Kusini(18), Sudan (14) na Djibouti ambayo itawakilishwa na waogeleaji 16. Pia kutakuwa na waogeleaji 48 kukamilisha jumla ya waogeleaji 263.
Waogeleaji hao watashindana katika staili tano tofauti za muogeleaji mmoja mmoja na pia kutakuwa na mashindano ya relei (relay). Jumla kutakuwa na matukio 140.
Waogeleaji wa timu ya Tanzanites ambao wamepewa jukumu la kuiletea sifa Tanzania katika mashindano hayo kwa upande wa wanawake ni Bridget Heep, Maryam Ipilinga, Crissa Dillip na Lorita Borega.
Wengine ni Amylia Chali, Filbertha Demello, Aminaz Kachra, Aliyana Kachra, Lina Goyayi, Sophia Latiff, Ria Save, Natalia Ladha, Sarah Tibazarwa, Muskan Gokan na Sarah Shariff.
Waogeleaji wanaume ni Julius Missokia, Max Missokia, Kabeer Lakhani, George Nangale, Austin Okore, Aryan BhattBhatt, Nabeel Gahhu na Mark Tibazarwa.
Wengine ni, Peter Itatiro, Delbert Ipilinga, Ethan Alimanya, Romeo Mwaipasi, Hilal Hilal, Collins Saliboko, Mohameduwais Abdulllatif, Michael Joseph na Aaron Akwenda.
Waogeleaji wa timu ya Diamond ambao watashiriki katika mashindano hayo ni Zainab Moosajee, Aamina Takim, Myra Makwaia, Abigail Mutungwa, Mahek Desai, Amaris Nanyaro, Catherine Maokola, Aaliya Takim, Mischa Ngoshani, Naisae Teggisa, Rahma Semizigi na Kalya Temba.
Kwa upande wa wanaume ni Kaysan Kachra, Hape Coleman, Alberto Itatiro, Luke Okore, Zac Okumu, Isaac Mukani, Enrico Barretto na Sahal Harunani. Wengine ni Christian Fernandes, Salman Yasser, Delhem Rashid, William Chengula, Elia Kimimba, Santo Bash,George Coleman, Nathan Kagoro, Sayi Goyayi, Elia Hangi na Revocatus Joseph.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Hadija Shebe alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kuwaomba wadau wa mchezo huo kujumuika kuipa sapoti timu ya Tanzania.