Mshambuliaji wa timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kulia akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ya Mkoani Arusha (TICD) leo wakati wa mechi ya mpira wa miguu ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Shimuta ambapo timu hizo zilitoka sare tasa ya kutokufungana
Mshambuliaji wa timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kulia akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ya Mkoani Arusha (TICD) leo wakati wa mechi ya mpira wa miguu ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Shimuta ambapo timu hizo zilitoka sare tasa ya kutokufungana
Mashabiki wa timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakifuatilia mchezo huo |
Na Oscar Assenga, TANGA.
TIMU ya Soka ya Shirika la Petroli Tanzania (TPDC) imelazimishwa sare tasa kutokufungana na timu ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ya Mkoani Arusha (TICD) katika mchezo wa mpira wa Miguu uliochezwa kwenye Dimba la Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Shimuta.
Katika mchezo huo ambao ulianza kwa kasi kwa kila upande kupambana kutaka kuvuna alama tatu ambapo walilazimika kushambuliana kwa zamu kila mmoja kwa kuonyesha umahiri wake.
Timu ya TPDC ambao walikuwa wakiongozwa na wachezaji wake mahiri Nahodha Dalushi Shija,washambuliaji wake Eugene Isaya,Kiungo mshambuliaji Mohamed Muya ,Joseph Samani na Dastan Masasi waliweza kusakata vema kabumbuku na kuwa mwiba kila walipokuwa wakigusa mipira uwanjani.
Hali hiyo ilipelekea timu ya TPDC kufika mara kwa mara langoni mwa wapinzani wao lakini bahati haikuwa yao ya kuweza kupata bao na hivyo kujikuta wakimbulia pointi moja.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo,Kocha Mkuu wa TPDC Matuka Bizoo alisema kwamba wanashukuru kwa kuanza na sare lakini sio kwamba wameridhika ila watakwenda kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ili kuweza kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye michezo mengine.
Bizoo alisema tatizo kubwa ambalo aliliona lililosababisha sare tasa hiyo ni timu yake kukosa muunganiko hivyo nalo atahakikisha analifanyia kazi haraka.
“Kikibwa leo niwapongeze angalau tumepata pointi moja sio mbaya lakini niwatake mhakikishe mnatulia mnapokuwa uwanjani na kupunguza presha “Alisema