Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza MPC Edwin Soko (wakwanza kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa kutoka Shirika la FAO
Wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza MPC wakiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Shirika la FAO
Afisa kutoka Shirika la FAO Omar Penarubia (wakwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za MPC
************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza (MPC) imepokea ugeni kutoka Shirika la chakula na kilimo la umoja wa Mataifa (FAO).
MPC imepokea ugeni huo leo Novemba 16, 2022 katika ofisi za klabu hiyo ambapo wamefanya mazungumzo ya namna watakavyo fanya kazi kwa pamoja na waandishi wa habari sanjari na kuweka mikakati ya kuwajengea uwezo juu ya kuandika habari za uhaba wa chakula kwenye mazao ya samaki.
Maafisa waliofika katika klabu hiyo ni Omar Penarubia na Julie Heye ambapo wamesema watashirikiana na waandishi wa habari katika kuhakikisha jamii inatambua umuhimu wa kuzingatia usalama wa chakula hatua itakayosaidia upotevu wa chakula kupungua.