Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akiwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Kanali Hamza Burah baada ya kufika Ubalozini na kufanya mazungumzo na Balozi huyo juu ya ujio wa Doris Mollel nchini Uganda.
Doris yupo nchini Uganda kwa mwaliko maalumu na anatarajiwa kuwa Mgeni wa heshima kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti kesho November 17,2022.