Na Mwandishi Wetu,Tanga
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga kwa kushirikiana na wadau wa usalama
barabarani wamezindua MpangoKazi wa Safari Salama na Endelevu kwa Jiji hilo
lengo likiwa ni kuwa mikakati endelevu wa kuendeleakupunguza ajali za
barabarani huku ikielezwa takwimu zinaonesha kwamba mwaka 2021 zaidi ya
asilimia 30 ya watu wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani , hivyo
kupoteza nguvu ngazi ya Taifa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango huo jana Mkuu wa Wilaya ya Tanga
Hashim Mgandilwaambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba ,
ameeleza kwamba mpango huo umelenga kupunguza ajali za barabara hadi kufikia
asilimia 50 ifikapo mwaka 2025 ambao unafadhiliwa na taasisi ya Amend kwa
ufadhili wa Botnar foundation.
Ameongeza kuwa ajali za barabara zimekuwa zikisababisha nchi kuingia
gharama kubwa kwa ajili yakutibu majeruhi wanaotokana nanajali hizo huku
familia zikiingia kwenye utegemezi jambo ambalowakati mwingine hupelekea athari
za kiuchumi kwenye ngazi ya familia hadi jamii.
Amefafanua kuzinduliwa kwa mpango huo ni sehemu ya mafanikio ya kupunguza
changamoto za ajali zabarabara hivyo iwapo wadau wote watashirikishwa na
kusimamiwa kwa ufanisi utaweza kuletamabadiliko makubwa ikiwemo kupunguza au
kumaliza kabisa changamoto za usalama barabarani.
“Mpango Kazi wa Safari Salama na Endelevu unakwenda kupunguza changamoto za
ajali, hivyoniwaombe Shirika la Amend kwa kushirikina na Jeshi la Polisi pamoja
na wadau wengine wanaohusika na miundombinu ya barabara zetu kuendelea kutoa
elimu ya usalama barabara kwa wananchi sambamba na watumiaji wa vyombo vya moto
kuheshimu alama za barabara sambamba na madhara yakuhujumu miundombinu
hiyo,”alisema Mgandiliwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo
amesema kwamba MpangoKazi wa Safari Salama na Endelevu kwa Jiji la Tanga
umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, Amend,
Fondation Botnar, wakala wa serikali wa barabara TANROADS na TARURA, shule za
msingi na sekondari, asasi za kiraia, vijana, mashirika ya kimataifa, sekta binafsi,
watumiaji wa barabara na wadau wengine. Haya ni matokeo ya ushirikiano endelevu
wa masuala ya usalama barabarani na usafirishaji ulioanza mwaka 2019.
“Mpango kazi huu umeanisha mikakati 10 ambayo imekubaliwa na wadau, na
fedha za utekelezajizimekwisha ainishwa hivyo utekelezaji wake umekwisha anza.
Mikakati ambayo imeanishwa ni pamojana kampeni ya usalama barabarani kwa umma
kupitia vyombo vya habari, kuwashirikisha wanasiasa kwenye masuala la usalama
barabarani, kuwashirikisha Maafisa Maendeleo ya Jamii kwenye kufikisha ujumbe
wa usalama barabarani kwa jamii, kuhamasisha uboreshaji wa miundombinu salama
yawatembea kwa miguu kwenye maeneo ya shule, kuanzisha na kusimamia maeneo
salama ya shule,kuimarisha elimu ya usalama barabarani mashuleni, kuhakikisha
njia za watembea kwa miguu zipo wazi bila kutumiwa na wafanyabiashara,
wajasiriamali, bodaboda na magari, kutoa mafunzo kwa maderevawa pikipiki, kutoa
mafunzo ya huduma ya kwanza mashuleni na kwa waendesha bodaboda, pia kuimarisha
ushiriki wa wadau wengine.
“Aidha Mpango umeainisha matarajio nane kupitia mijadala iliyohusisha wadau
mbalimbali ambayoitachangia kuleta manufaa ya muda mrefu. Katika kuongeza kasi,
tunatazamia ushirikiano wa karibu katiya serikali na sekta binafsi ili kugeuza
matarajio haya kuwa vitendo.
Matarajio hayo ni pamoja na kuhakikisha kuna ufadhili endelevu wa Mpango
Kazi huu, kupitia upya faini za makosa ya barabarani namatumizi mabaya ya
miundombinu, kuzingatia safari salama na endelevu katika mipango
miji,kurasimisha sekta ya bodaboda, kuimarisha ukaguzi wa vyombo vya moto,
kuboresha taa za mitaani na
barabarani, kuboresha mfumo wa kushughulikia matukio ya ajali za barabarani
na kukuza matumizi yateknolojia na ubunifu katika kuboresha usalama
barabarani,”alisema Kalolo.
Awali akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga
Inspekta George Elihakialisema kwa kushirikiana na Amend wameweza kutoa elimu
ya usalama barabara kwa waendeshabodaboda takribani 500 ndani ya Jiji hilo na
kupitia elimu hiyo imesaidia watumiaji wa vyombo vya moto
wakiwemo waendesha bodaboda kupunguza ajali za barabarani. “Kutokana na
kundi hili la bodabodakuwa miongoni mwa wahanga wakubwa wa ajili za barabara
tulianza na kutoa elimu kwao ili wawezekujilinda na ajali za barabara lakini na
umuhimu wa kuheshimu na kutii kanuni za usalama barabarani ili kujilinda wao na
watumijia wengine wa barabara hizo.”