*********************
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Novemba 14
HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani kwa kushirikiana na Shirika la Elimu Kibaha pamoja na Mji wa Gotland ya nchini Sweden zinatekeleza mradi wa Usawa wa jinsia ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya Dunia .
Katika utekelezaji wa malengo hayo Tanzania ni nchi moja wapo kati ya nchi 196 wanachama wa Umoja wa Mataifa zinazotakiwa kutekeleza malengo hayo.
Akizungumzia mahusiano kati ya halmashauri ya Mji wa Kibaha na Mji wa Gotland ,katika kikao Cha madiwani ,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Selina Wilson alieleza, wamejikita katika Mradi wa jinsia ni Lengo namba 5 ambalo linataka kuwe na usawa ambao hautomuacha nyuma msichana Wala mvulana.
Selina alieleza, mradi mwingine ni mradi wa Sekondari kwa Mji na Shirika la Elimu ili kuwawezesha wanafunzi kuelewa nchi inatekeleza malengo ya maendeleo endelevu.
“:;Lipo lengo linalosisitiza usawa katika elimu na kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike kujiamini na kuhakikisha wanakuwa miongoni mwa sehemu ya kuleta mabadiliko”
Nae mratibu kutoka Mji wa Gotland Eva Flemming alisema, wamekuja ujumbe wa watu nane ili kujifunza masuala mbalimbali ya shughuli za Halmashauri kwa kulinganisha na kwao.
Alisema,wametembelea pia shule ya Bundikani na Kibaha Sekondari kujionea mradi wa usawa wa jinsia na elimu Sekondari.
Awali mratibu wa safari kutoka maendeleo ya jamii Halmashauri ya Mji Kibaha, Anita Lyoka alifafanua tarehe 18-23 September mwaka huu timu kutoka Halmashauri hiyo ilisafiri kwa ajili ya kwenda kuhudhuria kikao Cha kamati tendaji ya usimamizi wa miradi ya uhusiano baina ya Mji wa Gotland na Kibaha.
“Tumejifunza mambo mengi ikiwemo kutokaa na utekelezaji wa Jambo ,hakuna masuala ya tunasubiri mchakato,”upangaji mzuri wa masoko mfano masoko ya mitumba ambayo mtu yeyote anaweza kwenda kuuza ama kutoa vitu asivyohitaji kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji”Hii inatunza Mazingira kwasababu watu hawachomi wala kutupa vitu hivyo”alieleza Anita.
Alitaja mambo mengine kuwa ni jamii ikielemishwa inaweza kubadilika na kutunza urithi wa rasilimali kwa faida ya vizazi vijavyo.
Anita alibainisha, mipango miji inazingatia utekelezaji wa Maendeleo endelevu ambapo Vijijini na mjini kumepangwa vizuri kwa nafasi na miundombinu ya barabara imeunganishwa maeneo yote, matumizi ya mabasi yanayotumia Nishati ya umeme yanasaidia utunzaji wa Mazingira na ushirikiano mzuri wa wafanyakazi na watendaji katika idara mbalimbali katika mji wa Gotland.
Mji wa Kibaha na Gotland Sweden ulianza mahusiano toka mwaka 2006.