************************
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Novemba 14
HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha, Mkoani Pwani, imekadiria kukusanya sh. bilioni 45.8 kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato yake katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Akisoma taarifa ya bajeti kwenye kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika Mjini Kibaha, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Selina Wilson amesema kuwa bajeti hiyo ya fedha ni ya Julai hadi Septemba mwaka huu.
Selina ameeleza ,fedha hizo zinatokana na vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ruzuku, mapato ya ndani na washirika wa maendeleo wa Halmashauri hiyo.
Amefafanua,hadi sasa makusanyo yaliyopatikana katika kipindi cha robo mwaka kuanzia Julai hadi Septemba kiasi cha fedha kilichokusanywa ni shilingi milioni 8.4 sawa na asilimia 18 ya makusanyo kwa kipindi hicho.