MSAJILI wa Bodi ya Usjali wa Wahandisi Nchini (ERB) Mhandisi Benard Kavishe ,akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 10,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na Mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka 2022/2023.
MSAJILI wa Bodi ya Usjali wa Wahandisi Nchini (ERB) Mhandisi Benard Kavishe ,akijibu maswali mbaimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 10,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na Mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka 2022/2023.
MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Habari -MAELEZO Gerson Msigwa,akizungumzia na waandishi na habari (hawapo pichani) kuhusu mazuri yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita mara baada ya Msajili wa Bodi ya Usjali wa Wahandisi Nchini (ERB) Mhandisi Benard Kavishe ,kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na Mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka 2022/2023 leo Novemba 10,2022 jijini Dodoma.
………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
BODI ya usajili wa Wahandisi Nchini (ERB) inatarajia kujenga kituo Kikubwa Cha Umahiri eneo la kizota, Jijini Dodoma ambapo ni Moja ya Vipaumbele vyake ili vijana waweze kufanya shughuli zao kwa kuonyesha ubunifu wao.
Hayo yameelezwa leo Novemba 10,2022 jijini Dodoma na Msajili wa Bodi hiyo,Mhandisi Bernard Kavishe ,wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo na Mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka 2022/2023 .
Mhandisi Kavishe amesema kutokana na kuwepo kwa Vijana wengi wenye mawazo ya kibunifu ila wanakosa namna ya kuendeleza mpaka kufika sokoni ,hivyo kituo hicho kitakuwa eneo sahihi la kuendeleza mawazo hayo.
“Kuna vijana wengi wenye mawazo mazuri kabisa ila namna ya kuendeleza inawawia vigumu sana ila tumeona sisi kama bodi suluhisho lake ni kujenga kituo cha umahiri ambapo itatumika kuendeleza vijana na Itakuwa na maabara pia,” Amesema Mhandisi Kavishe
Aidha Mhandisi Kavishe, amesema kuwa rushwa bado ni kikwazo kikubwa katika sekta hiyo nchini hali inayosababisha watu wasio na uwezo kupatiwa kazi katika maeneo mbalimbali.
“Rushwa bado ni kansa ya taifa katika maeneo mbalimbali kweli bado wapo watu ambao wanajihusisha na vitendo vya rushwa lakini sisi tunapo wabaini tunawafikisha katika vyombo vyenye mamlaka na suala hilo kama vile TAKUKURU na wengine”amesema Mhandisi Kavishe
Vilevile, Mhandisi Kavishe amesema kikwazo kingine wanachokabiliana nacho ni vishoka walipo katika sekta hiyo hivi sasa.
“Vishoka ni ‘crime’ kama ambavyo ilivyo katika tasnia nyingine mtu kujifanya Daktari wakati siyo taaluma yake anastahili kushitakiwa na kufungwa kama mharifu mwingine”amesema