Kaimu Mkurugenzi wa AfrONet, Constantine Akitanda akifutilia mkutano wa wadau wa mbegu asili.Mwenyekiti wa TOAM, Dk Mwatima Juma akizungumza na wadau wa mbegu asili waliokutana jijini Dodoma
***********
MWENYEKITI wa Shirika la Kuendeleza Kilimo HaiTanzania (TOAM), Dk Mwatima Juma amewataka wadauwa mbegu asili na zilizosahulika kujikita kwenye utafiti, ili kuweza kushawishi mamlaka kwanini wanataka mbeguhizo kupewa kipaumbele.
Dk Mwatima ametoa rai hiyo jana wakati akizungumza nawadau hao waliokutana kwa siku tatu jijini Dodoma katika kongamano la kujadili hatma ya mbegu asili nazilizosahaulika hapa nchini na duniani kwa ujumla.
Mkutano huu umeshirikisha wadau kutoka Shirika la SWISSAID Tanzania, Alliance for Food Sovereignty in Afrika (AFSA), TOAM, Shirika la Kuendeleza KilimoHai Barani Afrika (AFRONET), PELUM Tanzania, Mkulima Mbunifu, Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania (SAT), ECHO East Afrika na wengine.
Mwenyekiti huyo alisema kuzungumza na kuhamasishakilimo hai cha kutumia mbegu asili kila siku, kunawezakuwa na matokeo chanya iwapo kutakuwa na taarifa zakitafiti.
“Hawa wafanya maamuzi wana mambo mengi, jambo la kusisitiza na kuwabana ni sisi wadau wa mbegu asilikuonesha ushahidi wa kitafiti za kisayansi ambazozitaweza kuwashawishi kuweka mkazo katika eneo hilo,” alisema.
Dk. Mwatima alisema kila taasisi ambayo inahamasishamatumizi ya mbegu asili inapaswa kutenga fedha kwaajili ya utafiti, pamoja na kutoa elimu kwa wakulimaumuhimu wa mbegu hizo.
Alisema pamoja na utafiti ambao unatakiwa kufanyika nivema kuonesha athari ambazo ardhi imepata kupitiakilimo ambacho hakitegemei mbegu asili.
Mwenyekiti huyo alisema iwapo kundi hilo la mbegu asililitakuwa na misimamo ya pamoja katika kupigania kilimohai cha kutumia mbegu asili ni wazi kuwa ajenda hiyoitaweza kunusuru jamii na taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu waShirika la Kuendeleza Kilimohai Barani Afrika (AfrONet) Constantine Akitanda, amekieleza kikao cha wadau wambegu mjini hapa kuwa bara la Afrika lina kila sababu yakuzalisha chakula cha kutosheleza mahitaji ya watu wake wote.
“Ni lazima nchi ijielekeze katika kuongeza uzalishaji wamazao yaliyotelekezwa ama mazao yatima, mazao hayayana nutrisheni ya kutosha na ni miongoni mwa mazaoyanayohimili ukame, yanastawi hata katika ardhi isiyo narutuba ya kutosha na kuhimili magonjwa” alisema.
Akitanda alisema kufuatia mabadiliko ya tabianchikuendelea kuiathiri dunia, uzalishaji wa mazaoyaliyozoeleka kama mahindi, mpunga na ngano ambaokwa sehemu kubwa unategemea mvua, ni wazi kwambamahitaji ya kujitathimini ni makubwa zaidi ili kuwa namkatati thabiti wa kupanua wigo wa mazao yatima.
Tanzania kama zilivyo nchi nyingine za Kiafrika lazimaiwe mstari wa mbele ili isiachwe nyuma katikakujihakikishia usalama wa chakula siku za mbeleni.