Na.Abel Paul- Jeshi la Polisi
Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMONI MWANGAMILO amewataka maderva wa vyombo vya moto kuwa makini katika matumizi ya vyombo hivyo Pamoja nakufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara katika Mkoa wa Arusha.
Hayo yamesema leo November 08 2022 wakati wa kukabidhi pikipiki kwa viongozi wa dini kutoka Manyara,Kilimanjaro Pamoja na Arusha ambapo amesema kuwa viongozi wanaowajibu wa kutibu mionyo ya wanadamu kiroho ambapo amewaomba kutokubali kuvuta na shetani wakati wa matumizi ya vyombo hivyo.
SP Solomon amesema wao kama Jeshi la Polisi wanawajibu kutoa Elimu kwa makundi yote ili kuwa na uelewa wa Pamoja ili kukomesha ajali katika mkoa wa wa Arusha.
Kwa upandae wa Askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk BARNABAS MTOKAMBALI amesema lengo la kutoa vyombo hivyo ni kuwafikia waamini wa zehebu hilo nakutoa huduma ya kiroho na kazi za kanisa ikiwa ni Pamoja nakuongeza kasi ya maendeleo ya kanisa hilo
Wakati huo huo Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha SP SOLOMON MWANGAMILO amewata madereva wa vyombo vya moto maarufu mando wanaofanya safari zao nje ya jiji la Arusha na Kwenda maeneo ya vijijini kufanya marekebisho ya vyombo hivyo ili kupunguza ajali za mara kwa mara.
Ametoa kauli leo 08.11.2022 kata ya Meserani wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha alipokuwa anazungumza na maderva wa vyombo hivyo ambapo amewataka kufanya marekebisho na kufuata sheria za usaklama barabarani