Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt Ashantu Kijaji akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ya mafanikio ya utelekezaji wa Mpango wa Kuboresha Biashara na Uwekezaji,Mafunzo hayo yametolewa kwa Wahariri na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Jijini Dar es salaam.
Naibu katibu mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Bw. ALLY S. GUGU akiongea na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali leo katika mafunzo ya utelekezaji wa mpango wa kuboresha Biashara na uwekezaji. Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Ashanti Kijaji (alievaa kitambaa cha blue ) naibu katibu mkuu wa Wizara hiyo Bw. Ally S. Gugu wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi wahariri na waandishi wa vyombo vya habari walishiriki katika mafunzo hayo.
*********************
Na Anjela Seth
Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji nchini imeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuwafanya waweze kuwekeza kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Ashanti Kijaji wakati akifungua mafunzo ya Wahariri na Waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya utelekezaji wa mipango ya kuboresha Biashara ya uwekezaji.
Waziri Kijaji amesema kwamba serikali kupitia Wizara husika imekutana na watu wa sekta binafsi wenye viwanda na kuwaelekeza kuaandika kero zao ili Wizara iweze kuzishughulikia ambapo ameongeza kwamba kuanzia mwezi wa Desemba mwaka huu serikali inanzisha mchakato wa kubadilisha sheria zinahusu masuala ya kodi.
“Serikali ya awamu ya Sita(6) imeamua kufungua milango ya majadiliano na wawekezaji wa sekta binafsi kwa ajili kuzungumza, kujadiliana ili kupata majawabu mazuri kati ya serikali na sekta binafsi”amesema Waziri Kijaji.
Aidha ametoa maelekezo kwa Wahariri na Waandishi wa habari kushirikiana kwenda kutoa elimu kwa wananchi, wawekezaji na wadau mbalimbali kujitokeza kuwekeza kwani serikali ya awamu ya sita(6) imejipanga vyema kushirikiana nao.
Aidha amesema kuwa baadhi ya sheria zilizotugwa au kufanyiwa marekebisho ni usuluhishi wa migogoro, serikali imefuta kipengele (16)2 cha sheria ya makampuni ili kuondoa takwa la kugongewa muhuri na kamishina wa viapo, pamoja na marekebisho ya kifungu cha 60 cha sheria ya ushindani kinachohusu adhabu ya makosa ya ushindani ili ihusishe pato ghafi lililopatikana ndani ya Tanzania Bara na si duniani kote.
Hata hivyo amebainisha kuwa serikali imefanya mabadiliko ya sheria na kanuni mbali mbali kuondoa muingiliano wa majukumu ya Taasisi na mamlaka za udhibiti, miongoni wa muingiliano ulioondolewa ni pamoja na jukumu la kusimamia usalama wa chakula na vipodozi kutoka iliyokuwa mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) kwenda shirika la viwango Tanzania (TBS).
Waziri kijaji ameongeza kwamba Utekelezaji wa mpango wa kuboresha Biasharana na Uwekezaji (MKUMBI) inafuata misingi na utendaji wa kazi huku akitaja misingi inayopaswa kuzingatiwa katika utekelezaji wa (MKUMBI) ambayo ni pamoja na Maboresho yanayofanywa na mamlaka yasilenge kuongeza mapato bali kukidhi gharama za utoaji huduma ,ukusanyaji wa mapato kutumia nyenzo rahisi na rafiki kwa kuweka vituo vya pamoja vya huduma au kuunganisha mifuko
Misingi mingine ni kuondoa mwingiliano wa majukumu ya Taasisi kwa kuunganisha majukumu ambayo yanaingiliana
sheria, kanuni na taratibu zilenge kutekeleza sera za Biashara ushindani kumlinda mlaji na huduma za uma ,Udhibiti uwe wa kuendeleza sekta husika au uzalishaji ili kukuza ushindani wa kimkakati wenye usawa, tija na Ubunifu kwa kupunguza tozo na ada,kuwa na mifumo ya udhibiti yenye uhakika endelevu na inayotabirika.
Pamoja na kanuni zote zitakazotugwa zifanyiwe tathimini ya adhari ya uthibiti kabla kuidhinishwa kutumika kuhakikisha kuwa maboresho ya kupunguza kanuni hayaondoi mamlaka udhibiti kutatua changamoto za kiutendaji ndani na baina ya mamlaka za udhibiti.