Mpima Ardhi Mkoa wa Singida Sesaria Martin (katikati) akielekeza jambo wakati wa kukabidhi hatihizo
Na Dotto Mwaibale, Manyoni
WANANCHI Wilaya ya Manyoni mkoani Singida wametakiwa kuwa na Hati Milki za
maeneo yao ili kupunguza migogoro ya ardhi iliyopo katika wilaya hiyo.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa wakatiwa
hafla yakukabidhi hati kwa wananchi waliofanya mchakato wa kupima maeneo yao
nakuyalipia hafla iliyofanyika hivi karibuni wilayani humo.
“Migogoro mingi yaa ardhi wilayani hapa inatokana na wananchi wengi
kutokuwa na Hati milki za maeneo yao hivyo kuwa changamoto kubwa” alisema
Mwagisa..
Alisema kuna haja ya kila mwananchi
wa Manyoni kuwa na hati ya kiwanja na shamba ili kuhakikisha migogoro ya ardhi
inaisha kabisa au inapungua kwa kiasi kikubwa.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza
alisema mwitikio wa wananchi
kumilikisha maeneo yao kwa sasa umekuwa mkubwa kutokana na wananchi wengi kuwa
na uelewa mkubwa kuhusu hati miliki.
Hoza alisema wataendelea kutoa elimu
kwa wananchi kuhusu umhimu wa kuwa na hati miliki za maeno yao kwa mkoa mzima wa Singida ili
kuhakikisha kila mwananchi anakuwa nayo jambo litakalosaidia kupunguza migogoro
ya ardhi.
Alisema pamoja na mwitikio wa wananchi kuwa
mkubwa bado kuna changamoto kwa baadhi yao kwa kulalamikia gharama za
mchakato mzima unaofanyika kuwamilikisha maeneo yao.
Baadhi ya wananchi wameipongeza ofisi ya ardhi Mkoa wa Singida kwa
mchakatohuo na kueleza kuwa upatikanaji
wa hati hizo umekuwa rahisi tofauti na awali ambapo walilazimika kwenda Wizara
ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi jijini
Dodoma au Dar es Salaam kwa ajili ya
kuzipata.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wamesema changamoto iliyopo kwa sasa ni
wananchi wengi kuwa na uelewa mdogo wa wa faida za kuwa na hati milikihizo.
Zoezi la ugawaji hati hizo kwa
wananchi wa Wilaya ya Manyoni mkoani
hapa linafanyika baada ya wananchi kukamilisha taratibu zote za kisheria za
kupatiwa hati hizo.