*******************
Mbunge wa Tanga Mjini ambae pia ni Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu leo tarehe 5/11/2022 amezindua Mpango wa kutoa Huduma za Upasuaji wa Kibingwa bila malipo kwa wakazi wa Tanga.
Mpango huo ambao utasaidia kufanyika kwa upasuaji utakafanywa na Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Peleks Humanitarian Organisation ya nchini Uingereza ambapo jumla ya wagonjwa 380 watafaidika kati ya wagonjwa zaidi ya 700 waliofanyiwa uchunguzi (screening).
Kambi hii ya matibabu bingwa ya upasuaji imewezeshwa na Taasisi ya Watumishi Health Check, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo) na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini ambapo kwa pamoja wamewaleta wataalamu hao wa upasuaji kutoka Uingereza.
Akizungumza katika Ufunguzi wa Kambi hiyo Mh Ummy amesema kuwa Tanzania bado ina uhaba mkubwa wa madaktari bingwa hivyo mpango huu wa kambi ya Upasuaji wa huduma za kibingwa unajitaiika sana sio tu kwa Mkoa wa Tanga bali katika Mikoa yote nchini. Mhe Ummy amewashukuru Wataalam wa Peleks na Watumishi Afya Check kwa kudhamini Mpango huu ambao utasaidia wana Tanga na Watanzania kwa ujumla kupata matibabu,dawa vifaa tiba bila gharama yoyote.
Aidha Mkurugenzi wa Watumishi Afya Check Dkt. Siraji Mtulia ameeleza kuwa Upasuaji huo utafanyika kuanzia tarehe 5/11/2022 mpaka 11/11/2022 na utagharimu jumla ya shilingi milioni mia nane themanini na sita (mil. 876)
Hafla hiyo ya Ufunguaji ya Matibabu ya Upasuaji wa Kibingwa pia imehudhuriwa na Mkuu wa
Wilaya ya Tanga Mhe Hashim Mgandilwa; Naibu katibu mkuu wizara ya Afya Dr. Seif Shekalaghe, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe Abdulrahamani Shilloo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Wahe Madiwani na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Tanga.
Imetolewa na;
Ofisi ya mbunge Tanga Mjini.
5/11/2022.