Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua ugawaji wa vishikwambi katika sekta ya elimu kwenye ukumbi wa jiji Mtumba jijini Dodoma, Novemba 4, 2022. Kulia ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyaleu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, akitoa taarifa fupi ya ugawaji wa Vishikwambi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vishikwambi katika sekta ya elimu leo Novemba 4,2022 jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kishikwambi Mwalimu Victoria Kishiwa wa Shule ya Sekondari Dodoma wakati alipozindua ugawaji wa vishikwambi katika sekta ya elimu kwenye ukumbi wa jiji Mtumba jijini Dodoma, Novemba 4, 2022. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Adolf Mkwenda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kishikwambi Mwalimu Bernard Sinkamba ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Munguri Dodoma wakati alipozindua ugawaji wa vishikwambi katika sekta ya elimu kwenye ukumbi wa jiji Mtumba jijini Dodoma, Novemba 4, 2022. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Adolf Mkenda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kishikwambi Mwalimu Victoria Kishiwa wa Shule ya Sekondari Dodoma wakati alipozindua ugawaji wa vishikwambi katika sekta ya elimu kwenye ukumbi wa jiji Mtumba jijini Dodoma, Novemba 4, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa ugawaji wa vishikwambi katika sekta ya elimu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika uzinduzi huo kwenye ukumbi wa jiji Mtumba jijini Dodoma, Novemba 4, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa ugawaji wa vishikwambi katika sekta ya elimu wakiwa wamebeba vishikwambi walivyokabidhiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika uzinduzi huo kwenye ukumbi wa jiji Mtumba jijini Dodoma, Novemba 4, 2022. Kutoka kulia ni Mwalimu Hadikwa Chidumizi wa Shule ya Msingi Nkuhungu Dodoma, Mwalimu Victoria Kishiwa wa Shule ya Sekondari Dodoma, Mwalimu Mashaka Mnjalloh, Mdhibiti wa Ubora wa Elimu katika jiji la Dodoma, Mwalimu Robert Tesha, Afisa Elimu Kata ya Mnadani Dodoma na kulia ni Mwalimu Bernard Sinkamba ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Mnguru. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
***********************
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua ugawaji wa vishikwambi katika sekta ya elimu na huku ikionya matumizi yasiyosahihi ya vifaa hivyo.
Akizindua ugawaji wa vishikwambi hivyo leo Novemba 4,2022 jijini Dodoma Majaliwa amesema Serikali haitarajii kuona vitendea kazi hivi vinazagaa mtaani na pengine kumilikishwa kwa wasiohusika.
Amesema kuwaserikali imedhamiria kuwekeza kwenye Tehama hivyo vishikwambi viwafikie walengwa waliokusudiwa ili kuleta mapinduzi ya elimu nchini ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Tehama ya mwaka 2016.
“Nataka vifaa hivi viwafikie walengwa wote kwa wakati ili waweze kufanya kazi,hapa ningependa kusisitiza kwamba vifaa hivi ni kwa walimu tu na kweli viwafikie na kutumika na walimu na si vinginevyo,”amesema Waziri Mkuu
Aidha amewataka viongozi watakaopewa na jukumu la kugawa vishikwambi mikoani na wilayani hakikisheni hakuna mwalimu atakayekosa kishikwambi kwani idadi ya walimu na idadi ya vishikwambi tunazijua.
Majaliwa amesema lengo la ugawaji wa vifaa ni kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya TEHAMA.
”Naiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iimarishe ufundishaji wa somo hilo katika ngazi zote za elimu. ”amesema
Waziri Mkuu amewataka walengwa wote wahakikishe wanatunza vifaa hivyo na kuvitumia kwa malengo kusudiwa ikiwemo kusaidia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa zana mbalimbali za kufundishia na kujifunzia (rejea) kwa walimu.
“Tunaamini uwepo wa vifaa hivi utahamasisha sana matumizi ya teknolojia katika ufundishaji, kwa kutumia wataalamu wa ndani wa kila halmashauri uandaliwe utaratibu wa kutoa mafunzo ya msingi ya matumizi ya vifaa hivi, katika ngazi ya kata na wilaya,”amesema
Awali, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, amesema “Vishikwambi 300,000 vilinunuliwa kwa ajili ya sensa baadhi ya vishikwambi vilipelekwa Ofisi ya Takwimu kwa ajili ya zoezi la sensa ambapo Zanzibar vilipelekwa 6600 na 293,400 vilibaki Tanzania bara.”
Prof.Mkenda ameelezea mgawanyo wa vishikwambi hivyo kuwa ni walimu wa shule za msingi za umma 185,404, walimu wa shule za sekondari 89,805, Wathibiti Ubora wa shule ngazi ya Wilaya na Kanda 1,666, Wakufunzi wa vyuo vya ualimu vya umma 1393, Wakufunzi wa vyuo vya maendeleo ya wananchi 267, Maofisa Elimu Mikoa, Wilaya na Kata 5,772.
Pia amesema kwa Wakufunzi wa vyuo vya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi(VETA) vishikwambi 996 na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) Vishikwambi 8,357.
Hata hivyo ametaja faida mbalimbali za matumizi ya vishikwambi hivyo kuwa ni kupunguza gharama na matumizi ya karatasi, kusafiri na kurahisisha upatikanaji wa vyenzo za kujifunzia na kufundishia na usahihishaji wa mitihani.