Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), Mhe. Chief Fortune Charumbira akitoa ujumbe wa Mshikamano wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake leo Alhamis Novemba 3,2022.
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), Mhe. Chief Fortune Charumbira akitoa ujumbe wa Mshikamano wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake.
Na Kadama Malunde – Midrand Afrika Kusini
Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP) juu ya Haki za Wanawake umefanyika leo Alhamisi Novemba 3,2022 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini ambapo Rais wa Bunge la Afrika Mhe. Chief Fortune Charumbira akihamasisha nchi za Afrika kuwashirikisha wanawake katika utawala na ngazi za maamuzi.
Akitoa Ujumbe wa Mshikamano wakati wa mkutano huo ulioongozwa na mada isemayo ‘Uwezeshaji na ushirikishwaji wa wanawake katika utawala’, na kuhudhuriwa na wanaharakati wa haki za wanawake kutoka nchi mbalimbali, Mhe. Charumbira amesema ni vyema wanawake wakawezeshwa kwa vitendo badala ya kuwafurahisha tu wanawake kwa kusema wanawezeshwa.
“Bado wanawake hawajawezeshwa kikamilifu, bado kuna ni maneno tu. Ni lazima tuwawezeshe wanawake kwa vitendo. Je ndani ya uwezeshaji huu tunaoimba kila mara kuna nini?. Jinsia kwa uhalisia wake ni nini hasa? Tusiyatamke tu maneno haya (Uwezeshaji wanawake) kuwafurahisha wanawake kwa kusema tunawezesha wanawake, tufanye kwa vitendo mfano kwa kuongeza bajeti kwa masuala yanayohusu wanawake”,amesema Mhe. Charumbira.
“Lazima tuwaingize wanawake katika utawala, huku tukitambua kuwa utawala unaenda sambamba na masuala ya siasa hivyo wanawake waingie katika siasa. Tujiulize je kuna wabunge wangapi kwenye mabunge yetu ya nchi, kuna mawaziri wangapi?”,amesema Chifu Charumbira.
Ameongeza kuwa wanawake wanahofu kubwa na vitendo vya rushwa hivyo endapo watapata nyadhifa za uongozi vitendo vya rushwa vitapungua katika nchi za Afrika.
“Suala la rushwa limeturudisha nyuma sana kimaendeleo. Endapo tutakuwa na wanawake wengi katika maeneo mengi ya utawala na ngazi za maamuzi rushwa itapungua. Tukishirikisha wanawake katika masuala ya utawala tutasonga mbele”,amesema Rais huyo wa Bunge la Afrika.
Akizungumzia kuhusu mimba na ndoa za utotoni, Chief Charumbira amesema mimba na ndoa za utotoni bado ni tatizo kubwa katika jamii hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuchukua hatua ikiwemo kutunga sheria kali ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vinakatisha ndoto za watoto wengi.
“Watoto wa kike wameathirika sana na mimba na ndoa za utotoni ni wajibu wa kila mmoja wetu kuchukua hatua kudhibiti vitendo hivi”,amesema.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Tatu wa Bunge la Afrika, Mhe. Lucia Doss Passos amesema Wanawake wanatakiwa kushirikishwa katika ngazi za utawala lakini pia wawezeshwe kuwa na biashara, umiliki wa ardhi na kupata usaidizi wa kifedha na kuondoa kabisa ubaguzi wa kijinsia,kidini, kisiasa, na kiutamaduni.
“Wanawake wanachukua nusu ya idadi ya watu duniani lakini nafasi yao katika uchumi, kisiasa na utamaduni haioneshwi. Tunapaswa kuweka sheria ambazo zitaweka usawa wa jinsia ili kuleta usawa katika jamii. Wanawake wanatakiwa kupewa nafasi katika nyadhifa za uongozi na maamuzi”,amesema Mhe. Lucia.
“Wanawake wahusishwe katika maendeleo, wapewe elimu, kulindwa kiafya, kuwa na uwezo wa kifedha.Ili kuwa na jamii inayoheshimika lazima wanawake washirikishwe katika shughuli za maendeleo. Wanawake ndiyo wanaweza kuendeleza maendeleo”,ameongeza.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), Mhe. Chief Fortune Charumbira akitoa ujumbe wa Mshikamano wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP) juu ya Haki za Wanawake leo Alhamis Novemba 3,2022 katika ukumbi wa Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Makamu wa Rais wa Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), Mhe. Lucia Doss Passos akizungumza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake leo Alhamis Novemba 3,2022.