MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Erick Hamissi,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Kampuni hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Novemba 1,2022 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Erick Hamissi,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Novemba 1,2022 jijini Dodoma.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari maelezo Gerson Msigwa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasilishwa Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Novemba 1,2022 jijini Dodoma.
………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Erick Hamissi,ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 wametengewa na Serikali jumla ya shilingi Bilioni 111.8 kwa ajili ya ujenzi wa miradi 12.
Hayo ameyaeleza leo Novemba 1,2022 jijini Dodoma wakati akielezea Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Novemba 1,2022 jijini Dodoma.
Amesema kuwa Katika miradi hiyo 12 kuna miradi 4 ambayo ni mipya,miradi 5 ni ya ukarabati na miradi 3 inaendelea kutekelezwa tangu mwaka wa fedha uliopita.
Bw.Hamissi amesema kuwa kati ya hizo bilioni 111.8 Ziwa Tanganyika imetengewa kiasi cha Shilingi bilioni 53.9 itakayotumika kwa ajili ya kutekeleza miradi Mipya na kukarabati meli zinginine ikiwemo Meli Kongwe yenye miaka 105 ya MV Liemba.
“Katika ziwa Tanganyika kuna mradi mpya wa ujenzi wa Meli Mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo ambapo kwa mwaka huu wa fedha imetengewa jumla ya Bilioni 12,na mradi mwingine mpya kwa upande wa ziwa Tanganyika ni ujenzi wa Cherezo ambao nao umetengewa bilioni 12,
Na kuongeza kuwa ” Mradi mwingine mpya ni ujenzi wa Meli Mpya ya Mizigo tu ambapo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 3000 nayo imetengewa bilioni 12 kwa mwaka huu wa fedha,”Amesema Hamissi
Ameongeza kuwa katika ziwa Tanganyika wapo katika ukarabati wa Meli ya MT Sangara,MV Liemba ,MV Mwongozo ambayo inabeba idadi ya watu 800 na tani 80 ya mzigo pamoja na kukarabati Boti ya Kitalii ya Sea Warriors.
Kwa Upande wa Ziwa Victoria imetengewa kiasi cha Bilioni 59 ambapo kati ya hizo bilioni 24 zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa MV Mwanza Hapa kazi Tu ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 73.
Aidha amesema pia wataendelea na ukarabati wa Mv Umoja ambapo imetengewa Bilioni 1.7,Mv Ukerewe ambapo imetengewa bilioni 3.5 na ukarabati wa Meli ya Mafuta ya MT Nyangumi yenye uwezo wa kubeba lita 350 nayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 6.8.
“Tutajenga pia Meli nyingine Mpya kabisa ya Mizigo ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 3000 ambapo katika mwaka huu imetengewa bilioni 12 na hii itasaidia sana kuunganisha na Uganda yenye soko kubwa sana la bidhaa ambayo inahitaji zaidi ya tani elfu sita hivyo kukamilika kwa meli hii itasaidia sana nchi kuingiza mapato makubwa,”amesisitiza Bw.Hamissi
Bw.Hamissi amesema kuwa huduma ya usafiri kwa njia ya maji ni moja ya njia rahisi sana ndio maana serikali imeona umuhimu wa kuwekeza fedha nyingi ili kuimarishwa kwa miundombinu hiyo.
Pia Kampuni hiyo kabla ya kutetereka ilikuwa inaajiri zaidi ya vijana 300 ila baada ya kufa ila baada ya kufufuliwa tena kwa sasa ina wafanyakazi 120 ila miradi yote hii ikikamilika itaongeza idadi ya ajira na mapato pia yataongezeka kwa taifa.
Naye Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Habari MAELEZO Bw.Gerson Msigwa amesema kuwa serikali ya awamu ya sita mbali nakufanya juhudi za miradi ya ujenzi wa meli serikali pia inafanya uboreshaji wa bandari zote za maziwa makuu.