Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongella akisisitiza jambo na Mkuu wa chuo hicho ,Dk Mussa Chacha mara baada ya kuweka jiwe la msingi.Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongella akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa jengo hilo katika chuo cha ufundi Arusha leo
*************************
Julieth Laizer, Arusha.
Arusha.Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amekipongeza chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwa kujenga jengo la mradi wa Polyclinic kwa kizalendo,kitaalamu, na gharama nafuu na lenye ubora wa viwango vinavyohitajika.
Mongella ameyasema hayo Leo wakati akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa jengo la hospitali ya kufundishia na tiba la chuo hicho jijini Arusha.
Aidha amesema kuwa chuo hicho kimefanya kazi kubwa ya usimamizi wa mradi huo ambao utakuwa unatoa huduma za afya kwa wananchi,wanafunzi ambapo kwa uhalisia kazi hiyo itaijengea sifa chuo hicho ambapo amekitaka chuo hicho kujitangaza kwa kuwa kina utalaam wa kusimamia miradi kwa kutumia fedha za Force akaunti.
Awali akitoa taarifa ya mradi wa jengo hilo Mkuu wa chuo hicho Dkt.Mussa Chacha amesema Hospitali hiyo itatatua upungufu wa miundombinu ya kufundishia mafunzo kwa vitendo ya vifaa tiba (biomedical), tafiti na h.uduma bora za matibabu kwa wananchi wa Jiji la Arusha.
Hospitali hiyo inakadiriwa kutoa huduma kwa wagonjwa kati ya 100 hadi 300 kwa siku ikihudumia wanafunzi, wafanyakazi na wananchi wa Arusha kwa ujumla.
Pia kwa kuanzia itatoa huduma za uchunguzi wa afya, huduma ya
mama na mtoto, magonjwa ya macho, mfumo wa pua, koo na masikio, meno, magonjwa
ya ndani, huduma za upasuaji, huduma za utoaji dawa na vifaa tiba.
Hata hivyo ujenzi huo ilianza kutekelezwa November 1 ,2021 kwa njia ya force account na umejengwa kupitia mapato ya ndani ya chuo hicho na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.