Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga amesema michezo mbalimbali itakuwa kwa kasi katika Jimbo la Ismani kutokana na kuwepo kwa vipaji vingi vikubwa ya wanamichezo wanaopatika katika Jimbo hilo.
Akizungumza na blog hii, Kiswaga alisema kuwa amefurahishwa na vipaji vya mpira wa miguu na bao vilivyoonekana wakati wa sherehe za sababa zilizofanyika katika kata ya Ilolo Mpya Tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa.
Kiswaga alisema kuwa kuna vijana wanavipaji vikubwa hasa michezo ya jadi ambayo kwa kiasi kikubwa imesahaulika kwa kipindi kirefu hivyo amewaomba viongozi mbalimbali kuirudisha michezo hiyo.
Alisema kuwa mchezo wa Bao la solo limekuwa kiunganishi kikubwa kwa wananchi na serikali kama ambavyo hayati mwalimu Nyerere alitumia mchezo huo katika harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika na kufaulu kuupata uhuru huo.
Hivyo michezo yote inatakiwa kupewa kipaumbele sawa ili kuiweka jamii ya wanamichezo pamoja na kutumia fursa za michezo kwa maendeleo ya taifa.
Kiswaga aliwaomba wadau mbalimbali kuanzisha mashindano ya michezo katika Jimbo la Ismani ili kuendelea kuibua vipaji vipya vya wanamichezo wapya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa vijana wilaya ya Iringa vijijini,Elia kidavile alisema kuwa mchezo wa bao la solo ni mchezo ambao unachezwa na watu wa lika zote kwa ajili ya fursa na kutengeneza fursa za kimaendeleo wakiwa wanacheza mchezo huo.
Kidavile alisema kuwa mchezo wa bao la solo umekuwa moja ya michezo ambayo unatakiwa kutumia akiri nyingi na maarifa kuliko kutumia nguvu hivyo ukicheza mara kwa mara mchezo huo akili yako itachangamka kwenye kufikiri.
Aliowamba vijana kuucheza na kuenzi mchezo huo wa kitamaduni kwa kuondoa dhana ya kuwa mchezo huo ni wawazee tu na sio mchezo wa vijana.
Kidavile aliiomba serikali na wadau mbalimbali wa michezo kuwekeza katika wilaya ya Iringa kwa kuwa kunavipaji vingi vya wanamichezo ambavyo vinapotea tu bila ya sababu