Mtendaji Mkuu wa TBA,Arch.Daud Kondoro,akitoa maelezo kwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA) wakati wakikagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la OR.Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mtumba unaotekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la OR.Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhandisi Amon Nghambi akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA) baada ya kukagua Mradi wa ujenzi huo unaotekelezwa na TBA uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Ushauri Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch Dkt.Ombeni Swai,akitoa ushauri kwa Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la OR.Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhandisi Amon Nghambi mara baada ya Wajumbe wa Bodi hiyo kutembelea mradi huo unaotekelezwa na TBA uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Ushauri Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch Dkt.Ombeni Swai,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Wajumbe wa Bodi ya Ushauri TBA kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
MENEJA Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma, Victor Balthazar,akiwaeleza waandishi wa habari miradi wanayoisimamia mara baada ya Wajumbe wa Bodi ya Ushauri TBA kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la OR.Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora lililopo Mtumba Mhandisi Amon Nghambi,akizungumzia hatua ya ujenzi huo ulipofikia wakati wa ziara ya Wajumbe wa Bodi ya Ushauri TBA kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
Mradi wa Ujenzi wa Jengo la OR.Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora lililopo Mtumba ukiendelea unaotekelezwa na TBA
WAJUMBE wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA) wakimsikiliza Msimamizi wa uhandisi Mradi wa Nyumba 20 za Viongozi Nyumba 300 zilizopo Kisasa Mhandisi Immabaraka Shedafa wakati wa ziara ya bodi ya ushauri TBA kukagua miradi inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
MUONEKANO wa Mradi wa Nyumba 20 za Viongozi Nyumba 300 zilizopo Kisasa jijini Dodoma.
WAJUMBE wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA)wakipata maelezo ya Mchoro kutoka kwa Msimamizi wa mradi wa Ujenzi wa Nyumba 3500 zilizopo Nzuguni Bw.Fedrick Jackson mara baada ya wajumbe wa bodi ya ushauri wa TBA kutembelea miradi inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
MTENDAJI Mkuu wa TBA,Arch.Daud Kondoro,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA) kutembelea Miradi Mitano inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
MUONEKANO wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 3500 za Viongozi zilizopo Nzuguni unaotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
MUONEKANO wa Mradi wa Jengo la Kanda la Wakala wa Misitu (TFS) unaotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
Meneja Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma, Victor Balthazar,akitoa maelezo kwa Bodi ya Ushauri Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi Jengo la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unaotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
MUONEKANO wa Jengo la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linalotekelezwa na TBA jijini Dodoma.
…………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WAJUMBE wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA) wameipongeza TBA kwa kutekeleza kwa ubora miradi mbalimbali huku wakiiomba Serikali kuendelea kuupa kazi wakala huo.
Akizungumza Jijini Dodoma wakati wa ziara yao ya kukagua miradi inayotekelezwa na TBA Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa bodi hiyo,Dkt.Ombeni Swai ameupongeza wakala huo kwa kutekeleza kwa ubora miradi hiyo.
Miradi waliyotembelea ni pamoja na ule wa Wakala wa Misitu (TFS) jengo la Kanda,jengo la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),ujenzi wa nyumba 20 za viongozi wa Serikali na ujenzi wa jengo la ofisi ya Rais Utumishi Mtumba.
“Tumeona jinsi ambavyo miradi hii inasubiri hatua za mwisho wahusika kuhamia tumeona ubora wa kazi na tumeona ushirikiano wa timu kuanzia kwa Mkurugenzi Mkuu wa watu wengine.
“Tumeona timu ya wataalalmu, tumeona kazi nzuri na tunaimani sehemu zilizobakia zitakamilika kwa wakati,”amesema Dkt. Swai
Hata hivyo, Dkt. Swai ameiomba taasisi hiyo kuhakikisha inakabidhi miradi hiyo kwa wakati katika tarehe ambazo wamepanga ama ndani ya muda huo.
“Sisi kama bodi tupo tayari kushirikiana katika ushauri wa njia mbalimbali ili malengo yaweze kukamilika.Zaidi ya yote tunaishukuru Serikali kwa kuamini TBA.
“Tunaomba Serikali iendelee kutupa miradi hata watu waone kwamba tuna uwezo wa kufanya miradi mikubwa kama hii,”amesema Dkt. Swai
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TBA,Arch.Daud Kondoro amesema ushauri waliopewa na bodi hiyo wameupokea na wataufanyia kazi.
“Tumepata maelekezo mbalimbali binafsi nimeyachukua kwa maana ya kuyafanyia kazi tutakutana na wenzetu ili tuweze kutafsiri kwa vitendo,”amesema Arch.Kondoro
Naye, Meneja Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma, Victor Balthazar amesema wametembelea mradi wa Wakala wa Misitu ambao wanajenga jengo la kanda.
Amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 85 na unatarajiwa kukabidhiwa Novemba 27 mwaka huu.
Pia amesema wametembelea mradi wa Tanesco ambao umefikia asilimia 97 ya utekelezaji wake na ifikapo Novemba 22 mwaka huu jengo hilo liwe limekamika.
Amesema wametembelea ujenzi wa nyumba 20 za viongozi kwenye eneo la Kisasa ambapo amedai ujenzi huo unafanyika katika maeneo mawili ambayo wameyapa majina A na B.
Amesema kwa ujenzi wa eneo A ujenzi umekamilika kwa asilimia 100 na nyumba hizo tayari zimekabidhiwa viongozi na wamenza kuishi.
“Kwenye upande wa eneo B nyumba zipo sita nazo zimekamilika kwa asilimia 90 tunategmea ifikapo mwisho wa mwezi huu majengo hayo yawe yamekamilika kwa ajili ya matumizi,”amesema Meneja huyo wa mkoa wa Dodoma.