NA FARIDA MANGUBE, MAHENGE
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema kuwepo kwa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mahenge katika Mkoa wa Morogoro italeta manufaa mapana kwa Wachimbaji wa madini, wafanyabiashara wa madini pamoaj na Wananchi wa Wilaya ya Ulanga, Malinyi na Kilombero.
Dkt.Biteko ameyasema Oktoba 29, 2022 mkoani Morogoro wakati wa Uzinduzi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mahenge ambapo ambapo alisema kufunguliwa kwa ofisi hiyo kutatoa fursa kwa wachimbaji wakubwa na wadogo kupta huduma kwa ukaribu zaidi hali itakayosaidia kuongeza mapato.
Alisema kufunguliwa kwa Ofisi hiyo italeta tija kwa wachimbaji na wawekezaji kwani itaweza kusimamia na kuratibu kwa karibu shughuli zote za migodi kwa ukaribu zaidi tofauti na hapo awali ambapo huduma hizo zilikuwa zinapatikana na mjini Morogoro.
“Katika kipindi hiki ambacho migodi ya uchimbaji wa kati na mkubwa wa madini ya Kinywe (Faru Graphite Corporation) inategemea kuanza migodi hiyo, mbali na kutoa ajira kwa wazawa itasaidia kuinua uchumi na kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Jumla.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa a Morogoro Bi. Fatma Mwasa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Bi. Ngolo Malenya alisema kufunguliwa kwa ofisi hiyo kutaongeza usimamizi wa makusanyo pamoja na kutoroshwaji wa majini.
Alisema ya Wilaya Ulanga ina leseni za uchimbaji wadogo 203, wachimbaji wakati leseni 3, watafiti wa madini leseni 18 huku ikiwa na mchimbaji mmoja mkubwa na kufanya kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato kutoka milioni 314413168. Kwa mwaka wa fedha 2020-2021 na kufikia milioni 506245527.29 kwa mwaka wa fedha 2021-2022.alisema Alisema kwa kipindi cha mwezi julai na agost 2022 Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mahenge amefanikiwa kukusanya shilingi milioni 224 sawa na asilimia 22 ya lengo ya mwaka ya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni moja kwa mwaka wa fedha 2022-2023.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt. Dustan Kitandula amemshukuru Waziri Biteko kwa kuona umuhimu wa kuialika kamati katika ufunguzi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mahenge ambayo itasaidia kuongeza uwekezaji katika sekta ya madini.
Akizungumza katika ufunguzi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Adolf Ndunguru alisema kuwa Morogoro ni mkoa wa kipekee na umejaaliwa kuwa na madini ya kimkakati ya Kinywe, ambayo yana fursa ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi ya kuwezesha Sekta hii kuchangia asilimia 10 katika pato la taifa.
Awali Katibu Mtendani wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba alisema Mkoa wa kimadini wa Mhenge utasimamia wilaya tatu za Ulanga, Kilombero pamoja na Malinyi na kwamba utasimamia jumla ya leseni za dila 62, broker 68, leseni za uchimbaji mdogo 177 pamoja na mchimbaji mkubwa mmoja ambaye serikali imeitoa hivi karibuni.
Alisema kufunguliwa kwa ofisi ya afisa mkazi wa Mahenge kunaenda sambamba na uanzishwaji wa vituo vya ukaguzi wa madini katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Ulanga , Malinyi, pamoja na Kilombero.