Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,(Sera,Bunge na Uratibu) George Simbachawene,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na muongozo wa matumizi ya matokeo hayo leo Oktoba 28,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hamza Hassan Juma,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na muongozo wa matumizi ya matokeo hayo leo Oktoba 28,2022 jijini Dodoma.kushoto ni Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,(Sera,Bunge na Uratibu) George Simbachawene
………………
Na Alex Sonna-DODOMA
Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,(Sera,Bunge na Uratibu) George Simbachawene,amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kutangaza Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na muongozo wa matumizi ya matokeo hayo.
Hayo ameyasema amesemwa leo Oktoba 28,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Oktoba 31,2022 historia itaandikwa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma
Waziri Simbachawene amesema kuwa uzinduzi huo ni tukio muhimu katika historia ya maendeleo ya nchi ndio maana Serikali imeamua kuhakikisha kunakuwa na uwakilishi wa wananchi wa makundi yote ili waweze kushiriki katika tukio hili la kihistoria.
“Oktoba 31 ni siku maalum kwa taifa letu hivyo basi hatuna budi kuhakikisha kwa tuliopo Dodoma na mikoa ya jirani tunajitokeza kwa wingi uwanja wa Jamhuri na wale tutakaokuwa mbali tufuatilie uzinduzi huo kupitia vyombo vya habari ili tushiriki pamoja na Mheshimiwa Rais kujua tupo wangapi wakati atakapotangaza Matokeo hayo ya Mwanzo,”amesema
Simbachawene amesema kuwa katika zoezi hilo wegeni wengine ni pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Marais hao wastaafu watatunukiwa tuzo maalum kwa kufanikisha Sensa katika vipindi vya uongozi.
Ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa jirani kujitokeza kushuhudia uzinduzi huo na wahakikishe wanafika majira ya saa 12 kamaili asubuhi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hamza Hassan Juma amesema watakuwa na ujumbe wa watu zaidi ya 150 watakaoshiriki siku hiyo .
Juma amesema sensa ya mwaka huu ilifanikiwa kwa kiwango cha juu kwa sababu ya kuungwa mkono na viongozi wa kisiasa na kidini .