********************
Shamba linalomilikiwa na shule ya Sekondari Singe iliyopo Mjini Babati limechomwa moto na watu wasiojulikana.
Moto huo uliozuka jumatano oktoba 26,2022 majira ya Mchana licha ya kusababisha uharibifu kwenye Shamba la shule hiyo, pia ulihama hadi kwenye mashamba na Makazi ya watu na kusababisha taharuki Kubwa.
Jeshi la Zimamoto na uokoaji wilaya ya Babati kupitia kwa kiongozi Coplo Kahabi Mbupu, (Crew in charge) amesema Chanzo Cha Moto huo ni hujuma, ambapo kabla ya Moto kuwaka walionekana vijana watatu wenye umri kati 25-30 wakiwa kwenye shamba linalomilikiwa na Shule ya Singe Sekondari na Muda mfupi baadaye ulionekana Moshi eneo hilo na baadaye Moto ulisambaa maeneo mbalimbali ya shamba na eneo la makazi kulikokuwa na nyumba, shamba la migomba na bustani ya mboga na mifugo.
“Makazi yaliyoathiriwa ni eneo la Bw. Yuda Sandeu mwenye nyumba na shamba la migomba na bustani, na pia shamba la Shule ya Sekondari ya Singe” alisema
Aidha kiongozi huyo amewataka Wananchi wanapojenga nyumba kufuata ushauti wa wataalamu wa mipango miji ili kuoatikane nafasi ya barabara inayopitika kwa ajili ya huduma mbalimbali yakiwemo majanga ya moto na mengine.
“Licha ya kufanikiwa kuuzima Moto huo Changamoto iliyotukumba ni ukosefu wa barabara nzuri ya kufika eneo la makazi” alisema