Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Umma Ofisi ya Msajili wa Hazina, Lightness Mauki,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 26,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Zamaradi Kawawa,akizungumza mara baada ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kutoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 26,2022 jijini Dodoma.
……………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
HADI kufikia Juni 30, mwaka huu Ofisi ya Msajili wa Hazina imekusanya mapato yasiyo ya kodi ambayo yanajumuisha gawio, michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi na mapato mengineyo kiasi cha Sh. Bilioni 852.98 sawa na asilimia 109.5 ya lengo.
Hayo yameelezwa leo Oktoba 26,2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Umma Ofisi ya Msajili wa Hazina, Lightness Mauki,wakati akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Mauki amesema katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria pamoja na mambo mengine Msajili wa Hazina ana jukumu la kukusanya mapato yasiyo ya kodi ambayo yanajumuisha gawio, michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi na mapato mengineyo.
Bi. Mauki, Ofisi imeendelea kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi ambapo mapato yamekuwa yakiimarika mwaka hadi mwaka.
kuhusu upanuzi wa kiwanda cha sukari cha Kilombero amesema kuwa serikali ni mbia katika Kiwanda hicho ambapo ina umiliki wa asilimia 25 kupitia Msajili wa Hazina.
“Kutokana na kuendelea kukua kwa mahitaji ya sukari nchini sambamba na ongezeko la malighafi kutoka kwa outgrowers (wakulima wadogo wanaolima kandokando ya Mto Kilombero) kumekuwa na uhitaji wa kupanua kiwanda cha sukari Kilombero ili kutimiza mahitaji haya.