*Ukarabati
umekamilika, kinazalisha
*Kitasaidia
zaidi ya wakulima 3500
Na
Mwandishi Wetu, Lushoto
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF), Mhandisi Musa Iyombe amerBODI PSSSF YAKAGUA UKARABATI KIWANDA CHA CHAI MPONDEidhishwa na ukarabati uliofanyika katika kiwanda
cha Chai cha Mponde. Sasa kiwanda hicho kimenza uzalishaji.
Mhandisi
Iyombe alisema hayo mwishoni mwa wiki, ambapo yeye, akiongozana na wajumbe
wengine wa Bodi ya Wadhamini wa PSSSF walitembelea kiwanda hicho kilichopo
katika kijiji cha Kweminyasa,wilayani Lushoto ili kukagua maendeleo ya
ukarabati wa kiwanda hicho.
“Tumetembelea
kiwanda hiki cha Mponde ambacho kinazalisha chai bora, chai nzuri ambayo
inaweza ikatumika ndani na nje ya nchi. Kiwanda kipo vizuri baada ya ukarabati,
tumeona kiwanda kimeanza kuchakata majani ya chai, naamini wakulima wenye mashamba kwenye wilaya ya Lushoto, hususan Bumbuli, Korogwe na maeneo jirani watanufaika
sana na uwepo wa kiwanda hiki” alisema Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF.
Mhandisi
Iyombe alisema kuanza uzalishaji kwa kiwanda cha Chai Mponde ni wazi kwamba
vijana wengi watapata ajira na kwamba uchumi wa kata ya Mponde na wilaya ya Lushoto, ikiwemo Bumbuli na maeneo jrani utakuwa iwapo fursa ya kuwepo kwa kiwanda itatumiwa vyema.
Kwa
upande wake, Meneja wa Kiwanda hicho, Bi.Sane Kwilabya alisema, “kwa upande
wetu tumejipanga vyema kuzalisha chai bora katika kiwanda hiki, na tunaamini ardhi ya huku ni nzuri kwa kilimo cha majani ya chai yaliyo bora.”
Msimamizi
wa ukarabati wa mradi huo, Mhandisi Ally Shanjirwa alisema ukarabari wa kiwanda
hicho umekamilika kwa asilimia mia moja (100%) na sasa kinachofanyika ni kujaribu
mitambo ili kubaini dosari na kuzirekebisha.
Kiwanda
cha Chai Mponde kinaendeshwa kwa pamoja kati ya PSSSF na Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) kupitia kampuni ya Mponde Holding Company Limited, ambapo
kila Mfuko umewekeza asilimia 42 na Msajili wa hazina anamiliki hisa 16.
Kiwanda
kinategemewa kuzalisha ajira za muda mrefu zisizopungua 79 na ajira za muda
mfupi zinazokadiriwa kuwa kati ya 100 hadi 300 kutegemea na msimu wa mavuno ya
majani ya chai.
Uwepo
wa kiwanda cha Chai Mponde kitaongeza kipato kwa wakulima wa chai katika
Halmashauri ya Bumbuli na maeneo jirani, kuongeza mapato kwa taifa kupitia kodi
mbalimbali na kuongeza kipato cha fedha za kigeni kwa taifa kupita mauzo ya nje
ya chai ya Mponde.
Meneja
wa Kiwanda cha Chai Mponde, Bi. Sane Kwilabya (kulia) akitoa maelezo juu ya uzalishaji
wa chai kwa wajumbe wa Bodi ya PSSSF wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Musa
Iyombe (kushoto)
Mwenyeki
wa Bodi ya PSSSF, Mha. Musa Iyombe (kulia) akipata maelezo juu ya aina
mbalimbali za chai zinazozalishwa katika kiwanda cha Mponde kutoka kwa Menaja
wa Kiwanda hicho, Bi.Sane Kwilabya.
Wajumbe
wa Bodi ya PSSSF wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya kiwanda cha Chai cha
Mponde kilichokarabatiwa.