Mkuu wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora ,Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP),Advera Bulimba akitoa taarifa ya fedha zilizotolewa na serikali kwa kipindi hii na Serikali .
Jengo la dharula katika hospitali ya wilaya ya nzega mkoani Tabora ambalo ni moja ya mafanikio ya fedha hizo zilizotolewa na serikali kwa wilaya hiyo Mweneykiti wa CCM Wilaya ya Zzega Lt.(Mst) Maganga Sengerema akitoa neon kwenye Mkutano wa wadau wa maendeleo wilayani Nzega
************************
Na Lucas Raphael,Tabora
IKIWA ni takribani miaka miwili sasa Wilaya ya Nzega inajivunia utawala wa Rais wa awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan hasa katika kufanikisha kutekeleza miradi mbalimbali ya elimu, afya, maji, Umeme na miundobinu ya barabara.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega ACP Advera Bulimba wakati akitoa taarifa kwa viongozi mbalimbali wa serikali na siasa kwenye ukumbi wa halmashauri ya Nzega katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye wilaya hiyo ambapo alisema tangu machi 2021 mpaka sasa wilaya ya Nzega imepokea bilioni 97.3.
Awali ya yote alimpongeza Rais kwa jinsi anavyopambana katika kuhakikisha taifa la Tanzania linakuwa katika mazingira mazuri hasa kwenye Nyanja za Elimu kwa kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia.
Alisema katika awamu ya sita elimu msingi wilaya ya Nzega wamepata zaidi ya bilioni 2.98 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madasara 24, Madarasa ya shule sikizi 29 matundu ya Vyoo 64 pamoja na majengo ya Utawala.
ACP Bulimba alisema katika shule za Sekondari wamepokea kiasi cha bilioni 7.49 fedha ambazo zimetumika kujenga shule mpya za Sekondari 3, Vyumba vya Madarasa 252, Maabara 104, Matundu ya Vyoo 85 sanjari na miundombinu ya kunawia mikono.
Aidha alisema licha ya Rais Samia Suluhu Hassani kugusa kila sehemu ya maisha ya Mtanzania anayeishi wilayani hapo lakini amewezesha upatikanaji wa maji vijijini kwa zaidi ya asilimia 78 hadi kufika sasa.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Wilayani Nzega Eng.Faustin Makoka alisema mpaka sasa wamepokea bilioni 17.468 kwa ajili ya upanuzi wa maji ya ziwa Viktoria kwenda katika kata ya Mwamala, Itobo, Bukene, na vijiji vya kaloleni, Ilelamhi na na Mizibaziba.
Alisema kuna viijiji vingi ambayo tayari vinanufaika kwa kapata maji safi lengo kuu la serikali ya awamu ya sita likiwa ni kumutua ndoo mama kichwani kwani serikali ya awamu ya sita imedhamilia ifikapo 2025 huduma ya maji vijijini iwe imefikia asilimia 85.
Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Lt. Mst Maganga Sengerema alipongeza jitahada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa kiwango kikubwa hasa kwa kuangalia maeneo ambayo yanagusa maisha ya mtu mmoja mmoja.
Alisema hana shaka na utendaji wa Rais Samia hasa katika kusimamia na kutekeleza miradi mikubwa nchini jambo ambalo linapaswa kuungwa mkono na viongozi wote na watumishi kumsaidia kwa uadlifu mkubwa.
Nipende Kumpongeza Mkuu wa Wilaya hii ACP Bulimba amekuwa mfano wa kuigwa kwa jinsi ambavyo anamwakilishi Rais vizuri anasimamia vyema fedha zinazoletwa wilayani hapa anazitendea haki na ana uadilifu mkubwa.
Nao baadhi ya wananchi wa wilaya ya Nzega Suzana Juma, Ashura Idd, Sebron Juma na Jackson Ryoba kwa nyakati tofauti walimshukuru mkuu wa wilaya ya Nzega Bulimba kwa jinsi ambavyo amekuwa mstari wa mbele kuweka wazi fedha zote zinazotolewa na seriukali kwa shughuli za maendeleo katika wilaya ya Nzega.
Suzana alisema fedha hizo zimesaidia kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto katika wilaya hiyo ikiwemo barabara afya maji na kadhalika na kuongeza kuwa wao kama wananchi wataendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuangalia miradi yote ili iweze kudumu kwa muda mrefu.