NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum,Wakili Amon Mpanju,akizungumza wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini wa Wakuu wa vyuo, Manaibu wakuu wa vyuo, Wakufunzi na Waratibu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliofanyika kwa siku sita kuanzia tarehe 17-22 Oktoba 2022,jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum,Wakili Amon Mpanju,akifafanua jambo kwa washiriki (hawapo pichani) wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini wa Wakuu wa vyuo, Manaibu wakuu wa vyuo, Wakufunzi na Waratibu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliofanyika kwa siku sita kuanzia tarehe 17-22 Oktoba 2022,jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum,Wakili Amon Mpanju, wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini wa Wakuu wa vyuo, Manaibu wakuu wa vyuo, Wakufunzi na Waratibu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliofanyika kwa siku sita kuanzia tarehe 17-22 Oktoba 2022,jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Neema Ndoboka akitoa Maelezo ya mwenendo wa mafunzo wakati wa kufunga Mkutano wa wa Mwaka wa Tathmini wa Wakuu wa vyuo, Manaibu wakuu wa vyuo, Wakufunzi na Waratibu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliofanyika kwa siku sita kuanzia tarehe 17-22 Oktoba 2022,jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole Mbeya Bw.Rajab Kaleranda,akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini wa Wakuu wa vyuo, Manaibu wakuu wa vyuo, Wakufunzi na Waratibu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliofanyika kwa siku sita kuanzia tarehe 17-22 Oktoba 2022,jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum,Wakili Amon Mpanju,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini wa Wakuu wa vyuo, Manaibu wakuu wa vyuo, Wakufunzi na Waratibu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliofanyika kwa siku sita kuanzia tarehe 17-22 Oktoba 2022,jijini Dodoma.
…………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum Wakili Amoni Mpanju,amevitaka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini kuwapatia Vijana ellimu na ujuzi ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Wakili Mpanju ametoa wito huo leo Oktoba 22,2022 jijini Dodoma wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini wa Viongozi wa Vyuo na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo uliofanyika kwa siku Sita jijini Dodoma kuanzia Oktoba 17 hadi 22, 2022.
Mpanju amevitaka Vyuo na Taasi hizo kuweka kipaumbele katika dhana tatu za uwanagenzi, Maarifa na Ushirikishwaji wa jamii sambamba na kufanya tafiti huku akiwasisitiza kuzingatia Sheria, taratibu na Miongozo kwa Miradi inayo tekelezwa.
“Mhakikishe hizi dhana tatu za uanagenzi ambazo ni ushirikishaji wa jamii, ubunifu na maarifa mnaweka mikakati madhubuti ili kuendeleza na kusimamia maeneo hayo” amesema Mpanju
Aidha Mpanju amevitaka kuongeza nguvu katika maeneo yenye changamoto ambayo ni eneo Utafiti na huduma shirikishi na kama tatizo ni Bajeti itengewe kwa mwaka wa fedha ujao wa fedha na pia ninyi wawe na ushirikiano na vyuo vya ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo Mpanju amewaagiza wakuu hao Vyuo, Waratibu na Wakufunzi wa Vyuo kuhakikisa wanapinga na kukemea ukatili unaojitokeza na unaoendelea kushamili katika jamii kwa kuanzisha madawa ya Jinsia ili yaweze kusaidiana kupambana na vitendo hivyo.
“Tuna janga la ukatili wa wanawake na watoto, kitu ambacho kinaathiri nguvu kazi ya taifa na kuondoa amani kwa familia na Jamii, hivyo mnatakiwa muanze kuandaa midahalo yenye lengo la kujadili changamoto za jamii,muweke ushirikiano na serikali za Mitaa ili kuleta mabadiliko” amesema Mpanju
Aidha amewataka Wanafunzi kwenda kupanda miti mitano mitano kila mmoja pindi anapojiunga na Chuo huku akiwataka kuweka mipaka ya Chuo na kuhakikisha wanapata hati miliki kwa ambao bado hawajafanya hivyo ili kuepusha migogoro na jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Vyuo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Neema Ndoboka amesema lengo la kufanya mkutano huo ni kufanya tathmini ya mwaka kabla yakuanza kwa msimu Mpya wa Mwaka wa masomo ili waweze kuboresha utendaji kazi wa vyuo na kuleta matokeo change na tija iliyokusudiwa.
“Wizara imekua na taratibu ya kufanya tathmini kwa kuitisha vikao hivi kila mwaka kabla ya kuanza mwaka wa masomo ili kusaidia uendeshaji wa Vyuo vyetu vya Maendeleo ya Jamii kwa kubaini Changamoto na Kuweka maazimio yatakayoleta tija” almesema Ndoboka.