Baadhi ya wadau mbali mbali wa elimu wakiwemo walimu katika Manispaa ya Ubungo wakizungumza kwa nyakati tofauti juu ya ushirikiwao kàtika maadhimisho hayo yalioandaliwa na Shirika la Ocode.
……………………………
Na Victor Masangu,Mbezi
SHIRIKA isilokuwa la kiserikali la Organization for Community Development (OCODE) kwa kushirikiana na Shirika la Stromme foundation wameamua kushirikiana kwa pamoja kwa kuwakutanisha walimu na wanafunzi ili kuweka mipango madhubuti ya kusaidia kuinua kiwango cha elimu.
Mashirika hayo mawili yameamua kufanya hivyo lengo ikiwa ni kuwakutanisha kwa pamoja wadau hao wa elimu kutoka Manispaa ya Ubungo kwa lengo la kutoa mada mbali mbali zikiwemo kujadili maendeleo ya kitaaluma kwa walimu na ushirikishwaji wao katika utengenezaji wa mitaala ya elimu.
Kukutana kwa mashirika hayo mawili lengo lao kubwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu kwa wanafunzi pamoja na walimu wao kuwapatia mafunzo ikiwa ni sambamba na kusherekea maadhimisho ya mwalimu duniani ambao wao walichelewa kuzifanya kutokana na sababu mbali mbali.
Akizungumza katika sherehe hizo Meneja wa miradi ya elimu kutoka Shirika la Ocode Digna Mushi amebainisha kwamba leo la kuwakutanisha walimu na wanafunzi kutoka shule nne za msingi zilizopo katika Manispaa ya Ubungo lengo ikiwa ni kujadili kwa pamoja changamoto zilizopo pamoja na kuweka mikakati ya kusaidia kuboresha sekta ya elimu.
“Sisi Kama Ocode tumekutana hapa na wadau wetuu mbali mbali wa elimu wakiwemo walimu na wanafunzi kutoka shule nne za msingi zikiwemo,Kiluvya,Goba,Kibwegere pamoja na shule ya msingi malamba mawili na hizi zote zipo katika Manispaa ya Ubungo kwani ndio mradi wetu unatekelezwa,”Alisema Mushi.
Pia aliongeza kuwa lengo lingine la kukutana na wadau hao wameeza kuwasilisha mada mbali mbali juu ya kuwakumbusha walimu kuhusiana na utekelezaji wa majukumu yao katika kuwafundisha wanafunzi na kuona wana umuhimu gani katika jamii ambayo inawazunguka na wajitambue.
Mushi alibainisha kuwa ulimwengu wa sasa Kuna umuhimu mkubwa katika matumizi ya sayansi na teknolojia hasa kwa walimu lengo ikiwa ni kuongeza ufanisi zaidi katika kazi zao ambazo wanatakiwa wapatiwe mbinu za kumfundisha mtoto.
“Pia tumeweza kutoa mada tatu tofauti katika maadhimisho hayo yakiwemo jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya kimitaala,suala la changamoto ya kusoma,kuhesabu na kuandika (KKK) na mambo mengine ya ushirikishwaji wa walimu katika masuala ya elimu,alifafanua Mushi.
Katika hatua nyingine alisema Shirika la Ocode limekuwa likiendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wa maendeleo katika kukabiliana na changamoto ya miundombinu ambapo jitihada zao kubwa ni kuendelea kujenga vyumba vya madarasa ya awali kwa ajili ya watoto kupata fursa ya elimu ikiwemo kuwawekea zana za kufundishia.
Kwa Upande wake Kaimu afisa elimu Manispaa ya Ubungo Asha Mkomwa ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika kufungua maadhimisho hayo amelipongeza shirika la Ocode kwa kuwakutanisha walimu na wanafunzi pamoja kwa lengo la kujadili masuala yanayohusiana na sekta ya elimu.
“Kikubwa ambapo nimekipenda katika siku ya leo no Ocode kuweza kutambua mchango mkubwa na kazi ambayo inafanywa na walimu wa manispaa ya Ubungo na kuamua kuwapatia zawadi mbali mbali ikiwa kama ni motisha katika kuwafundisha wanafunzi,”alisema Asha.
Aliongeza kuwa tangu Shirika hilo lianze kutekeleza mradi wa elimu umeweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa kuwasaidia watoto waweze kujua kusoma,Kuhesabu na kuandika na kwamba kumeleta matokeo chanya zaidi katika suala la elimu katika Manispaa ya Ubungo.
Sara alitoa wito kwa mashirika mengine kuiga mfano wa Ocode katika kusaidia elimu na kwamba wanapaswa kutembelea katika maeneo ya shule ili kuweza kubaini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika.
Naye mmoja wa mwalimu aliyeshiriki katika maadhimisho hayo akiwemo Boke Mwita kutokea shule ya msingi malamba mawili amesema kitendo walichokifanya Ocode ni hatua kubwa ya kuweza kuinua na kufikia malengo katika nyanja ya elimu na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.
Shirika la Organization for Community Development ((OCODE) limekuwa likitekeleza miradi mbali mbali ya elimu katika Manispaa ya Ubungo na kwamba katika sherehe za maadhimisho hayo imetoa zawadi kwa walimu ambao wanafanya vizuri lengo ikiwa ni kuwapa motisha na molali katika kufundisha wanafunzi.