Picha mbalimbali za mahafali ya 15 Shule ya msingi Mwanalugali…
…………………..
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
WAZAZI na walezi wameaswa kujenga tabia ya kuwekeza akiba ya fedha kwa ajili ya watoto wao kwa kutumia Taasisi za kifedha ili kuwasaidia kuwaendeleza elimu ya juu na maisha yao baadae.
Aidha wazazi wametakiwa kuwaendeleza watoto kielemu ili kufikia elimu ya juu badala ya kuwa kikwazo cha kuwakatisha masomo kutokana na sababu zao,Jambo linalosababisha kukatisha ndoto za watoto.
Akitoa rai hiyo kwa wazazi,walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Mwanalugali ,Kibaha Mkoani Pwani, wakati wa mahafali ya 15 ,Grace Kalinga akimwakilisha Flaviana Msilu kutoka CRDB Bank PLC,Palm Beach Premier alieleza ,wapo wazazi walionufaika kutokana na kuweka kwa ajili ya watoto wao kipindi kirefu ambapo sasa wanawasomesha kupitia akiba hizo.
“Tusijisahau sana ,maisha yetu ya Sasa yanaweza kubadilika baadae,leo unacho kesho unaweza ukawa huna ,hivyo tujifunze kuweka kidogo tunachokipata ili kutukomboa miaka ya baadae”alifafanua Kalinga.
Aidha alieleza ,tawi hilo la Taasisi ya kifedha limejitolea kuwaanzishia Junior akaunt wanafunzi 12 katika shule ya msingi Mwanalugali zitakazosaidia wazazi wao kuziendeleza .
Awali Mwalimu mkuu shuleni hapo, Hambari Mshana alieleza,shule inafanya vizuri kitaaluma na kufaulisha kwa asilimia 92 mwaka 2019, asilimia 100 mwaka 2020 na mwaka 2021 asilimia 95.
Hata hivyo anasema, shule Ina changamoto ya Ukosefu wa vifaa vya Tehama ambavyo vingesaidia maandalizi ya mitihani,upungufu wa samani na vyumba vya madarasa.
Mshana alieleza, Serikali ilitoa milioni 23 kwa ajili ya ukarabati vyumba vya madarasa 3 ,choo cha walimu .
Mhitimu Prisca Mussa alishauri kuwepo na upatikanaji wa Chakula shuleni ili kupunguza utoro.
Waliahidi kulinda nidhamu waliyofundishwa wakiwa shule na kujiepusha na makundi yasiyofaa ikiwemo uvutaji bangi na panyaroad.