MAKAMU Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela,Prof.Emmanuel Luoga,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 20,2022 jijini Dodoma.
MAKAMU Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela,Prof.Emmanuel Luoga,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 20,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa,akizungumza mara baada ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kutoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 20,2022 jijini Dodoma.
…………………………..
Na Alex Sonna-DODONMA
TAASISI ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ipo katika hatua za mwisho kuingiza sokoni mfumo wa kubaini machapisho ya wizi ambapo mfumo uliokuwa ukitumika katika vyuo vingi ni wa kutoka nje na wa gharama kubwa.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 22,2022 jijini Dodoma na Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof.Emmanuel Luoga,wakati akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Prof. Luoga amesema kuwa Taasisi hiyo imejikita katika matumizi ya TEHAMA ambapo itapata Dola za Marekani milioni 10 mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia, fedha hiyo itatumika kuimarisha mifumo ya TEHAMA na kuhakikisha inapata ithibati ya maabara ya viwango vya kimataifa.
“Taasisi imejikita katika kuboresha ufundishaji kwa kutumia teknolojia ya masafa (e-learning) kwa waadhiri na kupanua wigo kwa wanafunzi walio mbali na kampasi kupata elimu ya masafa,”amesema Prof.Luoga
Amesema kuwa mpaka sasa taasisi imefanya bunifu 73 ambazo ni matokeo ya ushirikiano wa hali ya juu kati ya wahadhiri na wanafunzi pamoja na Serikali na wadau wa maendeleo kutoka nje ya nchi.
“Katika masuala ya utafiti na ubunifu, mpaka sasa taasisi yetu imefanikiwa kufanya bunifu 73 ambazo ni matokeo ya ushirikiano wa hali ya juu kati ya wahadhiri na wanafunzi pamoja na Serikali na wadau wa maendeleo kutoka nje ya nchi,”Amesema Prof.Luoga
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa serikali inafanya kazi kubwa kuandaa wanasayansi kutoka shule za msingi mpaka shahada za kwanza ambapo kwa sasa inajenga shule moja ya sekondari ya masomo ya sayansi kwa kila mkoa kwa ajili ya wasichana.
“Naipongeza taasisi hii kwa kutilia mkazo maalum kwenye kutoa elimu ya sayansi kwa wanawake,”amesema Msigwa
Aidha Msigwa ametoa wito kwa vyuo mbalimbali nchini kuweka kozi za umahiri kwa Waandishi wa Habari ili wakafanye tafiti za kutosha, hivyo kuondokana na kutoa habari za uongo na zisizokuwa na tija kwa umma.