Meneja Masoko wa Halotel, Sakina Makabu (Kulia) pamoja na Meneja Mahusiano na Stella Pius ( kwanza Kushoto), Mkuu wa shule ya Sekondari Bangulo ( Pili kulia), Diwani wa kata ya Pugu Station Mh; Shabani Musa ( katikati) na Mwenyekiti wa Serikal ya Mtaa wa Bangulo ( Pili Kushoto) kwa pamoja wakibeba moja kati ya Samani zilizotolewa kwa Shule ya Sekondari ya Bangulo Dar es Salaam wakati wa tukio la kukabidhi Vifaa hivyo leo kama moja ya msaada na muendelezo wa mkakati wa kuisaidia sekta ya Elimu ikiwa Kampuni hiyo ikiendelea kuadhimisha miaka Saba ya kutoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini.
Meneja Masoko wa Halotel Sakina Makabu akiongea na waandishi wa habari leo katika shule ya Sekondari Bangulo iliyoko wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo katika tukio la kukabidhia vifaa mbali mbali vya shule kwaajili ya kuboresha mazingira ya Waalimu ofisini na kuongeza ufanisi wa walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza ikiwa ni moja ya msaada kutoka kampuni ya simu ya Halotel katika kuendana na kuadhishimisha Miaka saba (07) ya Kampuni hiyo kutoa huduma za Mawasiliano hapa nchini.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bangulo Bw. Hussein Ramadhani Mwamtuya akiongea na waandishi wa habari leo katika shule ya Sekondari Bangulo iliyoko wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo katika tukio la kukabidhia vifaa mbali mbali vya shule kwaajili ya kuboresha mazingira ya Waalimu ofisini na kuongeza ufanisi wa walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza ikiwa ni moja ya msaada kutoka kampuni ya simu ya Halotel katika kuendana na kuadhishimisha Miaka saba(07) ya Kampuni hiyo kutoa huduma za Mawasiliano hapa nchini.Diwani wa Kata ya Pugu Station Bw; Shabani Musa akiongea na waandishi wa habari leo katika shule ya Sekondari Bangulo iliyoko wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam katika tukio la kukabidhia vifaa mbali mbali vya shule kwaajili ya kuboresha mazingira ya Waalimu ofisini na kuongeza ufanisi wa walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza ikiwa ni moja ya msaada kutoka kampuni ya simu ya Halotel katika kuendana na kuadhishimisha Miaka saba(07) ya Kampuni hiyo kutoa huduma za Mawasiliano hapa nchini. Afisa Elimu wa Sekondari wilaya ya Ilala Bw; Gerald Kwingwa akiongea na waandishi wa habari leo katika shule ya Sekondari Bangulo iliyoko wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam katika tukio la kukabidhia vifaa mbali mbali vya shule kwaajili ya kuboresha mazingira ya Waalimu ofisini na kuongeza ufanisi wa walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza ikiwa ni moja ya msaada kutoka kampuni ya simu ya Halotel katika kuendana na kuadhishimisha Miaka saba(07) ya Kampuni hiyo kutoa huduma za Mawasiliano hapa nchini. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Bangulo Bw. Goodluck Mwele akiongea na waandishi wa habari leo katika shule ya Sekondari Bangulo iliyoko wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam katika tukio la kukabidhia vifaa mbali mbali vya shule kwaajili ya kuboresha mazingira ya Waalimu ofisini na kuongeza ufanisi wa walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza ikiwa ni moja ya msaada kutoka kampuni ya simu ya Halotel katika kuendana na kuadhishimisha Miaka saba(07) ya Kampuni hiyo kutoa huduma za Mawasiliano hapa nchini.
**************************
Dar es Salaam,Oktoba 20, 2022 Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel hapa nchini imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya masomo kwa waalimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Bangulo ili kupunguza changamoto za mahitaji ya vifaa vya elimu zinazowakabili.
Akitoa taarifa hiyo leo wakati wa kukabidhi vifaa hivyo katika shule hiyo Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Sakina Makabu, amesema wameamua kusaidia vifaa hivyo kutokana na changamoto zinazozikabili shule hiyo.
Aidha, Sakina amesema mpango huo ni kuunga mkono juhudi za serikali ambazo zimekuwa katika kuhakikisha shule zote nchini zinapata mahitaji na vifaa muhimu vitakavyowezesha wanafunzi kupata elimu katika mazingira bora ili kukuza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi hao na katika kupunguza uhaba wa vifaa vya elimu kwa shule zote nchini.
“Halotel tumeamua kutoa msaada huu wa vifaa ambavyo ni meza na viti vya waalimu, kabati la vitabu na mafile, desktop mbili na printer ikiwa ni mojawapo ya muitikio wa kampuni yetu wa kuitikia juhudi za serikali katika uboreshaji wa mazingira na upatikanaji wa vifaa vya ufundishaji na kujifunzia ili kuongeza ufanisi wa kufundishia na kujifunzia katika mfumo wa nadharia na vitendo”. Aliongeza Sakina.
Pamoja na hilo, Halotel inatoa huduma ya kimasomo ijulikanayo kama ‘Halostudy” hili ni huduma ya kujisomea mtandaoni inayowawezesha wanafunzi kusoma mitaala ya masomo mbalimbali nchini kwa njia ya mtandao (TEHAMA) inayopatikana kwenye simu za mkononi na kwenye kompyuta ambapo wanafunzi na walimu kote nchini wanatumia bure,hivyo kupitia kompyuta tulizotoa leo Shule ya Sekondari Bangulo itaweza kutumia huduma hii kwenye kompyuta hizi.
Vile vile hatujaishia kwa shule za sekondari tu, kwa sasa tuna mpango mpya wa kuboresha zaidi sekta hii kidigitali kwa ngazi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vyote hapa nchini. Huduma hii itawawezesha wanafunzi wote vya vyuo vikuu hapa nchini kuweza kuwekewa vocha yenye thamani ya Tsh 1,500 kila mwezi.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Bangulo Bw. Hussein Ramadhani Mwamtuya alisema, “ Tumefarijika sana kwa kupokea msaada huu kutoka Kampuni ya simu ya Halotel, tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa karibu na jamii na kuthamini lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za kuisaidia sekta ya elimu nchini. Ninaamini kabisa vifaa hivi vitawasaidia walimu na wanafunzi hapa shuleni katika kuboresha namna ya ufusnishaji na kujifunza kwa ujumla”.
Halotel itandelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine wa elimu katika kuhakikisha na kufanikisha kusonga mbele sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kutengeneza wanafunzi bora wanaosoma masomo ya sayansi hasa kuelekea ukuaji wa uchumi wa viwanda.