*********************
Afisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments Fred Msemwa amewaomba wawekezaji kujitokeza ili kuchangia fursa ya Mfuko mpya wa “Faida Fund “ambao umeanzishwa na shirika hilo ili kusaidia wawekezaji kupata faida nakwamba fedha zao zipo salama.
Mkurugenzi Msemwa ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wadau wa uwekezaji wa mfuko wa faida Fund ambao unasimamiwa na Watumishi Housing pamoja na Benki ya CRDP Plc ikiwa ni kuwezesha Watanzania kuwekeza kwa kununua hati fungeni kwa bei nafuu kuanzia elfu 5000, nakuendelea.
Amesema kua mkutano huo umewakutanaisha wadau wa sekta za fedha ikiwemo Benki takribani 50 zilizopo hapa nchini, mawakala wa soko la hisa Dar es salaam ( DSE).
Amesema kuwa Watumishi Housing Investments inauza vipande vya mfuko wa Faida Fund kwani bado kuna fursa kubwa kwenye Masoko ya fedha hivyo mtu au kampuni itakayowekeza atanufaika na mfuko huo.
” Huu mfuko unafunguliwa rasmi tarehe moja mwezi Novemba, usalama wa mfuko huu ni mkubwa kwani unasimamiwa na kuidhinishwa na mamlaka ya serikali ya mitaji na Masoko CMSA, pia kutakua na mfumo maalum wa kufanya malipo kwa mitandao ya simu, au mwekezaji anaweza kwenda moja kwa moja kwenye ofisi za Benki au ofisi za Watumishi Housing Investments” amesema.
Amesema kuwa usimamizi wa kisheria wa Mfuko wa “Faida Fund” utasinamiwa na serikali kwani, nakwamba wawekezaji wanaweza kubaki kwenye uwekezaji wake milele au wanaweza kuacha pale watakapoamua mfuko kuufunga.
” Tunawekeza kwa miezi miwili ya mwanzo tunafunga , tunafungua tena miezi mitatu tunafunga baada ya hapo mwekezaji ataamua mwenyewe kuuza sehemu ya asilimia ya fedha aliyowekeza unaruhusiwa bila shaka yoyote.
Kwa upande wake Mkuu wa Masoko na Mitaji kutoka Benki ya CRDB PLC Masumai Ahmed Hashimu amewahakikishia wawekezaji kuwa fedha zao watakazoziwekeza kwenye Faida Fund zitakua salama nakwamba ni wakati sasa wa Watanzania kutumia mfuko huo kupata utajiri.