Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael akieleza jambo mbele ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof. William Anangisye wakati akitembelea mabanda ya watafiti na wabunifu katika Ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es SalaamKatibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael akizungumza jambo mara baada ya kutembelea moja ya banda la wabunifu DUCE katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael akitembelea baadhi ya mabanda ya wabunifu DUCE katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE),Prof.Stephen Maluka akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Baadhi ya wadau wa elimu wakiwa katika ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael akiwa na baadhi ya viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam wakipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa elimu katika Ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
CHUO Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kimetakiwa kutengeneza mkakati maalumu wa kuwawezesha wahitaji wa Chuo hicho kuwa na uwezo wa kujiajiri kwa kutegemea elimu na maalifa ambayo wameyapata Chuoni.
Wito huo umetolewa leo Oktoba 19,2022 na Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, hafla ambayo imefanyika Chuoni DUCE.
Amesema wahitimu wengi wapo mtaani wakisubiri kuajiriwa na hata wengine wamekuwa hawana uelewa wa kujiajiri lakini kama chuo kikitengeneza mikakati ambayo itaweza kumsaidia muhitimu kujiajiri basi vijana wengi watapata ajira.
Aidha Dkt.Francis amewapongeza wanataaluma wa DUCE na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuhakikisha wanafikia malengo wanayojiwekea kama taifa, hususani kwenye sekta ya elimu.
“Natambua kabisa ugumu wa kazi hii kwa kuwa nimeifanya mwenyewe kwa miaka mingi. Pamoja na ugumu huo, bado mmeendelea kuwa imara katika kutekeleza majukumu yetu”. Amesema Dkt.Francis.
Pamoja na hayo amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa elimu ya juu kwenye maendeleo ya taifa letu na ngezeko la bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ni moja tu ya mifano michache ya nia njema ya serikali ya kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu ya juu.
Amesema ni wajibu wa vyuo vikuu nchini kufanya tafiti mbalimbali, zikiwemo tafiti kuhusu namna ambayo elimu ya juu itakidhi matakwa ya sasa ya jamii ya kitanzania.
“Mna wajibu wa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mwelekeo wa sasa wa kitaifa na kimataifa na kisha kutafakari ni namna gani vyuo vyetu vitawawezesha wahitimu kuendana na mwelekeo huo”. Amesema
Nae Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE),Prof.Stephen Maluka amesema katika kipindi cha miaka 17, Chuo kimepata mafanikio mbalimbali na kutoa mchango mkubwa kwa taifa ikiwemo kushuhudia idadi ya wanafunzi wahitimu kuongezeka kutoka 522 Mwaka 2008 yalipofanyika mahafali ya kwanza, hadi kufikia wahitimu 16,330 Mwaka 2021.
Aidha, amesema katika mahafali ya 14, Mwaka 2021, idadi ya wahitimu ilikuwa 1,565, ikiwa ni idadi mara tatu zaidi ikilinganishwa na idadi ya wahitimu wa kwanza Mwaka 2008. Wahitimu hawa wamesaidia sana kupunguza uhaba wa walimu na wataalamu wa elimu nchini.
Amesema Chuo kimekuwa ni mahali pa kuchochea ubunifu unaowezesha wahitimu wetu kutatua tatizo la ajira kwa kuajiri na kuajiri watu wengine. Aidha, kutokana na kuwa na wanataaluma wabobezi katika fani mbalimbali, Chuo kimeweza kufanya tafiti mbalimbali zinazotatua matatizo ya jamii ya na pia kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu katika maeneo ya elimu, insia, sayansi na sayansi jamii.
Prof.Maluka ameeleza kuwa Chuo kimekuwa kikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo gharama kubwa ya usomeshaji wa wanataaluma ili wafikie kiwango cha Ph.D., ambacho hasa ndicho kinatakiwa kwao.
“Ili kukabiliana na changamoto hii, Chuo kimeendelea na utaratibu wake wa kusomesha wafanyakazi kwa awamu kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani, kutumia fursa za ufadhili kupitia vyuo rafiki nje ya nchi na kuomba uwezeshaji kutoka Serikalini”. Amesema Prof.Maluka
Amesema Chuo kimekuwa na uhaba wa vyumba vya kufundishia na kujifunzia, maktaba za TEHAMA zenye vifaa vyote muhimu na ofisi za watumishi wa Chuo na katika changamoto hizi, wanaishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuwasaidia katika usomeshaji wa baadhi ya watumishi wa Chuo na ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya Chuo kupitia miradi yake mbalimbali.