Matukio mbalimbali Pichani yakimuonesha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus M. Wambura pamoja na ujumbe alioambatana nao akiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Thailand, Maj. Gen. Khemmarin Hassir, ambapo tarehe 19 Oktoba, 2022 yalifanyika mazungumzo ya kujadili maeneo ya ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Thailand.
IGP Camillus M. Wambura na ujumbe wake alioambatana nao, wapo New Delhi nchini India, kuhudhuria mkutano Mkuu wa INTERPOL. Picha na Jeshi la Polisi