Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga akizungumza katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika Shule Kuu ya Elimu (SoED) pamoja na uzinduzi wa sera ya UDSM ya kuhudumia wafanyakazi wenye ulemavu na mahitaji maalumu iliyofanyika leo Oktoba 18,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga akizungumza katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika Shule Kuu ya Elimu (SoED) pamoja na uzinduzi wa sera ya UDSM ya kuhudumia wafanyakazi wenye ulemavu na mahitaji maalumu iliyofanyika leo Oktoba 18,2022 Jijini Dar es Salaam.Amidi ,Shule Kuu ya Elimu,Dkt. Eugenia Kafanabo akizungumza katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika Shule Kuu ya Elimu (SoED) pamoja na uzinduzi wa sera ya UDSM ya kuhudumia wafanyakazi wenye ulemavu na mahitaji maalumu iliyofanyika leo Oktoba 18,2022 Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye pamoja na Amidi ,Shule Kuu ya Elimu,Dkt. Eugenia Kafanabo wakiwa katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika Shule Kuu ya Elimu (SoED) pamoja na uzinduzi wa sera ya UDSM ya kuhudumia wafanyakazi wenye ulemavu na mahitaji maalumu iliyofanyika leo Oktoba 18,2022 Jijini Dar es SalaamNaibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye pamoja na Amidi ,Shule Kuu ya Elimu,Dkt. Eugenia Kafanabo wakipata picha ya pamoja na wadau wa elimu katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika Shule Kuu ya Elimu (SoED) pamoja na uzinduzi wa sera ya UDSM ya kuhudumia wafanyakazi wenye ulemavu na mahitaji maalumu iliyofanyika leo Oktoba 18,2022 Jijini Dar es Salaam
**********************
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga amesema sababu kubwa ya kuachwa nyuma kwa baadhi ya makundi kwenye jamii ni kukithiri kwa mifumo kandamizi na ya kibaguzi ikiwa ni pamoja na ubaguzi kwa misingi ya ulemavu ambapo inaziacha familia nyingi na jamii kwa ujumla ikiwa imetengwa.
Amesema hayo leo Oktoba 18,2022 katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika Shule Kuu ya Elimu (SoED) pamoja na uzinduzi wa sera ya UDSM ya kuhudumia wafanyakazi wenye ulemavu na mahitaji maalumu .
Amesema UDSM Kupitia kitengo chake maalumu cha kuhudumia wanafunzi wenye mahitaji maalumu wamekuwa mfano wa kuigwa kwani wamewezesha Chuo kutekeleza kwa vitendo malengo ya millennium,ahadi ya ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu na usemi wake maarufu wa usimwache mtu nyuma”leave no one behind”
“Usemi wa usimwache mtu nyuma una maana ya kuwafikia makundi maalumu/masikini kinaendelea,kuleta usawa na kuondoa ubaguzi miongoni mwa jamii pamoja na kuangalia visababishi vya umasikini na ubaguzi,na mambo yanazozuia usawa katika nchi au taasisi” Amesema Kipanga.
Aidha amekipongeza chuo kikuu cha Dar es salaam kupitia shule kuu ya elimu kwa kuwezesha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi wote,hasa wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Wizara ya elimu inatambua mchango na juhudi hizo katika utoaji huduma kwa jamii.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye amesema Chuo kimekuwa kikiwahudumia wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa kuzingatia ubora wa elimu sawa kwa wote na kukuza umahiri na kuzingatia sera ya elimu ya Chuo inavyotaka.
” Katika wa masomo Mwaka 2020/2021chuo kilidahuri wanafunzi wenye ulemavu 48 wanaume 24 na wanawake 24 na idadi ya udahiri imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka” Amesema Anangisye
Nae Amidi ,Shule Kuu ya Elimu,Dkt. Eugenia Kafanabo amesema katika maadhimisho hayo kutakuwa matukio mawili ambayo ni kongamano ambalo litajadili changamoto zinazowapata wanafunzi wenye mahitaji maalumu na namna ya kuzitatua, tukio la pili ni matembezi ya hiyari yanayolenga kuhamasisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu kuwa wanaweza kusoma na kufikia ngazi ya Elimu ya juu bila tatizo lolote.
” Mwaka 1978 chuo kilianza kutoa huduma kwa wanafunzi kwa wanafunzi wawili wenye ulemavu wa macho na mpaka kufikia sasa chuo kinazaidi ya wanafunzi 150 ambao wapo kwenye makundi mbalimbali ya ulemavu”. Amesema Dkt.Kafanabo
Aidha changamoto iliyopo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ni vifaa vya kujifunzia, miundombinu,usafiri,vifaa vya mawasiliano, mazingira ya elimu pamoja na maswala ya afya.